![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Ajitumbukiza chooni kwa kukwepa mbaroni11/09/2008
MTUHUMIWA wa makosa ya mauaji, Rashid Kibati (35), aibuka kutoka kwenye shimo la choo kwa lengo la kujificha.
MTUHUMIWA wa makosa ya mauaji, Rashid Kibati (35), Baada ya kutolewa chooni akidhibitiwa na askari kanzu na askari wa kikosi cha zimamoto mkoa wa Morogoro. Picha na gazeti la Mwananchi na Mpoki Bukuku. SHUGHULI za Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro juzi zilisimama kwa saa tatu baada ya mshitakiwa kutumbukia chooni kwa nia ya kujiua kukwepa kesi ya mauaji inayomkabili. Mshitakiwa huyo, Rashid Salumu Kibati (35) mkazi wa Kijiji cha Gonja, tarafa ya Turiani, wilaya ya Mvomero alifanya kituko hicho akiwa mahabusu kabla ya kesi yake kutajwa. Inadaiwa kuwa mahabusu huyo alimuomba askari aliyekuwa zamu Pc Elias kwenda kujisaidia na askari huyo akamsindikiza mpaka kwenye mlango wa choo hicho na kumuacha aingine peke yake. Askari huyo aliendelea kusubiri nje, na alipoona mshtakiwa hatoki ndipo alipopata wasiwasi na kuamua kuingia ndani. Alipoingia alipigwa na butwaa kwa kushindwa kumuona mshtakiwa na mpaka mshtakiwa alishindwa kuendelea kukaa chooni na kuamua kuibuka mwenyewe.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||