Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Gordon Brown a-ahidi mabadiliko na maisha bora

23/09/2008

WAZIRI mkuu wa UK Bw. Gordon Brown atimiza mwaka mmoja katika ofisi (10 Downing Street) tangu achukue nafasi ya kuwa kama Waziri Mkuu wa UK. Bwana Gordon Brown amekiri katika mkutano wa chama cha Labour uliofanyika Manchester kuwa matokeo ya uchaguzi mdogo (by-election) uliopita ulikuwa si wa kuridhisha kwa chama cha Labour ingawa ni dhahiri kabisa mabadiliko ya kiuchumi ya nchi hayakusababishwa na chama hicho.

Kama alivyosema waziri Ben Bradshaw wa (Labour) baada ya kushindwa katika kitongoji chake cha (Henley-on-Thames) kuwa, kushindwa huko sio kwa sababu ya uongozi wa Gordon Brown bali ni sababu ya uchumi ambao umekumba hali ya kiuchumi dunia nzima na si UK peke yake. Aliendelea kusema, hali mbaya hii ya kiuchumi si ngeni kwa chama cha Labour ambayo ishawahi kutokea miaka ya nyuma lakini kutokana na uongozi mzuri wa Labour wamewezesha kurudisha hali ya kiuchumi kama kawaida na kuwa bora zaidi.

Ingawa hali hiyo ya kiuchumi haikusababishwa na chama cha Labour au bwana Gordon Brown, Diwani wa Oxfordshire bwana Howell amesema wapiga kura wa Henley-on-Thames wameonyesha kuwa wanahitaji mabadiliko ya hali ya kimaisha na kufikiriwa kwa sheria mpya ya Road Tax.

Mbunge wa Reading West wa (Labour), Bwana Martin Salter ambaye pia alisaidia katika kusimamia uchaguzi mdogo wa Henley alisema, matokeo haya ya kushindwa katika uchaguzi huu ni sawa sawa na yale yaliyotokea Winchester miaka miwili iliyopita wakati wa Tony Blair na katika uchaguzi uliofuata tukashinda uchaguzi huo huo.

Bwana Gordon Brown amekiri katika mkutano wa (Labour) wa mwaka 2008 uliofanyika mjini Manchester kuwa kufanikisha mabadiliko ya kiuchumi na hali za kimaisha za watu, tutasikiliza nini watu (wananchi) wanataka. Aidha kwa kushindwa kwa uchaguzi mdogo, alisema, "by-elections come and by-elections go".

Bwana Brown aliendelea kusema katika mkutano huo, kazi yake kubwa hivi sasa ni kuangalia na kuhakikisha huduma nzuri kwa watu (public services), kurudisha na kukuza hali ya kiuchumi, kuhakikisha kuwa watu wanapata na wanafaidika huduma za afya na elimu ambazo watu wanataka na ataendelea kufanya hivyo kwa mafanikio ya watu.

Aliongeza kwa kusema, anajua watu wanajua hali ya kiuchumi hivi sasa ilivyo, na kazi yake kubwa ni kuiongoza nchi katika hali hii ngumu ya kiuchumi kuelekea katika hali nzuri ya kiuchumi.

Alisema, watu wanakabiliwa na bili kubwa za petroli, bili za gesi na umeme, bei kubwa za chakula na kazi yake kubwa ni kuhakikisha kufanya kila awezalo kuinua hali za watu za kimaisha kuwa nzuri.

Bwana Gordon Brown ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika kuchangia kuiongoza nchi na kuleta maendeleo ambayo yanaonekana dhahiri, alisema katika mkutano Manchester kuwa atapigana katika hali hii ngumu ya kiuchumi na alisema kwa uzoefu wake, "This is no time for a novice".

Bwana Brown amesema, ana mpango wa watoto ambao hawafanyi vizuri shule wasidharauliwe na kuachwa nyuma. Watoto wote watasaidiwa kwa mpango maalum na kuhakikisha kila mtoto haachwi nyuma katika masomo.

Bwana Brown amesema, amekiri kuwa watu wameona kama amewasiliti kwa kutangaza (10p tax) na ameahidi kurekebisha bili hiyo kwani amesema kama waziri mkuu, angependa kusaidia mapato ya kila familia na kuleta maisha bora kwa kila familia.

Kutokana na uzoefu wake, bwana Brown ameahidi kuleta mabadiliko ya kipesa ya dunia nzima (Global Financial System) mbali na mfumo wa kipesa unaotumiwa hivi sasa ambao anataraji akiwa katika uongozi wake utaleta manufaa ya uchumi bora na anataraji nchi nyingine duniani wataiga mfumo huo mzuri ambao utakuwa hapa UK.

Vilevile, Bwana Gordon Brown ameahidi kwa mpango alionao kutokomeza ufukara kwa watoto wa Great Britain ifikapo mwaka 2020 na aliahidi atatoa huduma za elimu ya watoto bure (nursery education) kwa watoto wote wenye miaka 2, 3 na 4. Alisema, "That's the fairness parents want, and that's the fairness every Labour party member will go out and fight for".


 

Maswali na Majibu ya kupiga kura nchini UK bonyeza hapa

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©