Kivukoni kuwa mambo mkeka
25/09/2008

UJENZI
wa kivuko kipya cha Kigamboni utakamilika katikati ya mwezi ujao na
kuanza kutoa huduma za usafishaji wa abiria na mizigo kati ya Feri
Magogoni na Kigamboni, Dar es Salaam.
Hatua
hiyo inatokana na kukamilika kwa ujenzi kivuko hicho kwa kiwango cha
asilimia 95. Kauli hiyo ilitolewa leo hapa Dar na Meneja Mwendeshaji,
Fuad Saadun, kutoka Kampuni ya Ujerumani ya Neue Ruhrorter Schiffswerft
GMBH wakati akiwaeleza maofisa habari na mawasiliano kutoka wizara
mbalimbali waliokwenda kuangalia hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa
kivuko hicho.

Alisema
kazi ya ujenzi wa kivuko hicho imekamilika kilichobaki ni kuweka nyaya
za umeme, kupaka rangi pamoja na kuweka viti kwa ajili ya abiria.
Saadun
alisema kivuko hicho kinachotengenezwa na kampuni hiyo ya Kijerumani,
kina uwezo wa kubeba tani 500 ambapo kitakuwa kikichukua abiria 2,000 na
magari 60 kwa wakati mmoja.
Alisema
kivuko hicho kimeundwa katika hali inayoruhusu abiria kutumia njia zao
katika kuingia ndani na kutoka tofauti na zile za vyombo vya usafiri.
|