Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

News archive

 01 January 2008

Happy New Year 2008

Watu laki saba walihudhuria sherehe ya mwaka mpya 2008 katika mitaa ya London, ambayo haijawahi kutokea kufikia namba hiyo miaka iliyopita. Wengi wao walikuwa katika ufukwe wa mto Thames (river Thames) wakishuhudia mripuko wa fataki ambazo zilipambwa katika jicho la London au (London eye) na huku kengele ya Big Ben ikilgonga kukaribisha mwaka mpya 2008. Matayarisho hayo ambayo yalitayarishwa na serikali, ambayo yalidumu kwa muda wa dakika 11 na kugharimu karibu milioni moja na laki mbili paundi (£1.2million).

Serikali ya U.K. iliandaa maaskari wa ulinzi wapatao 3,600 katika kulinda usalama wa raia kutokana na kutarajia watu wengi kukua kila mwaka katika maonyesho hayo ya mwaka mpya ya 2008 ambayo hufanyika katika kitovu cha London.

Vilevile, wengine walijazana Trafalgar square ambapo kulikua na maonyesho ya peke yake. Sana la Nelson liliwashwa taa na kumurika eneo lote la Trafalgar square. Maaskari walitanda kuzuia watu wasiingie zaidi ndani ya Trafalgar square ili kuepukana na kufurika kwa watu katika uwanja huo.

Mpaka kufikia saa kumi usiku, polisi waliwatia mbaroni karibu watu hamsini kwa makosa tofauti, yakiwemo ulevi, utovu wa nidhamu na fujo. Na watu 22 walikamatwa na mapolisi wa usafiri wa 'Underground' na mabasi.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©