![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS archive |
||||||||
|
|
06 January 2008 |
|||||||
Gordon Brown aitisha usuluhisho Kenya
Bwana Gordon Brown amesema, serikali ya UK inafanya kazi usiku na mchana kusuluhisha machafuko hayo kwa kuwapatanisha viongozi wa serikali ya Kenya. Zaidi ya watu 300 wamefariki mwezi uliopita katika machafuko yaliyoletwa baada ya uchaguzi wa urais ambao ulishindwa na Mwai Kibaki. Inasemekana hali hiyo inaweza kuzidi kuwa mbaya kwasababu inaelekea kwenye vita vya ukabila. Bwana Odinga ambaye alikuwa akigombea urais dhidi ya Mwai Kibaki, amekubali wito wa bwana Gordon Brown kukutana na kuzungumzia mapatano kati ya vyama hivyo. Rais wa Ghana John Kufuor, ambaye ni kiongozi wa umoja wa Afrika anatarajiwa katika mazungumzo hayo kuwa kama mmoja wa wasuluhishi. Watoa huduma wamesema, hali ya watu inazidi kuwa mbaya. Karibu watu 250,000 hawana pa kukaa wala hawana chakula bora. |
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||