Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS archive

 
 

 11 January 2008

Jipatie balbu za kusevu umeme wako na mfuko wako

Kuanzia leo mpaka tarehe 13/01/2008, Jumapili, unaweza kubadilisha balbu zako za kawaida za umeme na kujipatia balbu mpya za kusevu umeme kwenye duka lolote katika maduka 28 ya B&Q, London.

B&Q ikishirikiana na British Gas katika kampeni hiyo ambayo imezinduliwa rasmi kwa siku tatu na meya wa London, Ken Livingstone, ni katika juhudi za kupunguza utumiaji wa umeme ambao kisayansi unaathiri dunia (Global warming) na kusevu bili yako ya umeme.

Imesemekana kuwa, kila mkazi wa London akiwa na balbu hizo mpya za kusevu umeme, London itakuwa imesevu tani lakin tano za 'carbon emissions' na £139 milioni kwa mwaka.

Kila balbu inamsevu mwenye nyumba £7 kwa mwaka, kwahivyo kama una balbu 10 nyumbani kwako unasevu £70 kwa mwaka kwenye bili yako ya umeme. Vilevile balbu hizi mpya zinadumu mara 12 zaidi ya balbu za kawaida na zinatumia asilimia 20 ya umeme wa balbu ya kawaida. Kwahivyo unasevu asilimia 80 ya umeme kwenye kila balbu.

Angalia: B&Q watatoa balbu mbili (2) tu kwa kila mkazi wa London ambaye atakayekwenda kubadilisha balbu hizo. Aina ya balbu ni Philips.

Kutafuta anuani ya duka la B&Q ambalo lipo karibu na wewe London, bonyeza hapa.

Zenjydar Community Association

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©