Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS archive

 
 

 12 January 2008

Sherehe za miaka 44 ya mapinduzi ya Zanzibar

JK akiwa ameongozana na mama wa kwanza Bi Salma Kikwete, akigongesheana na mmoja wa maelfu ya watu waliohudhuria sherehe za miaka 44 ya mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amani.

Hapo hapo, rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Aman Abeid Karume ametoa msamaha kwa wafungwa 25 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 44 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, kifungu cha 59 kina mpa Rais uwezo wa kutoa msamaha kwa mfungwa yeyote kwa kumuachia kuwa huru au kumpunguzia adhabu.

Misamaha kama hiyo imeanza kutolewa na kiongozi wa awamu ya mwanzo marehemu Abeid Amani Karume ambapo ilikuwa kila zifikapo sherehe za Mapinduzi baadhi ya wafungwa waliokuwa wakistahili kwa mujibu wa sheria walikuwa wakipata msamaha.

Msamaha huo umewahusisha wafungwa mbalimbali kutokana na vigezo tofauti vikiwemo uzee, maradhi, waliobakisha muda mfupi kumaliza kifungo chao, wanaofuata maadili mazuri, wafungwa wasioweza kufanya kazi kutokana na uzee au ugonjwa na wengineo.

Msamaha huo hautawahusu wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa makubwa yakiwemo, waliopatikana na hatia ya biashara ya madawa ya kulevya, unyang`anyi wa kutumia silaha, ubakaji na waliofungwa kifungo cha maisha.

Mapinduzi ya kwanza ya Zanzibar yalifanyika Januari 12, 1964 baada ya utawala wa Sultan wa Oman na yaliongozwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar huru, marehemu mzee Abeid Karume.

Mapinduzi hayo ndiyo yaliyozaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Aprili 1964 na kupatikana Taifa la Tanzania chini ya uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©