![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Mafuriko ya Msumbiji14/01/2008
Mafuriko ya maji yamevamia miji na vijiji vya Msumbiji na kuuwa wakazi wa sehemu hizo. Wawili waliouwawa, wameuwawa kwa kung'atwa na mamba. Idara maalum ya mipango ya dharura ilitumia helikopta na maboti kuokoa watu 50,000 waliokumbwa na mafuriko hayo sehemu mbalimbali. Siyo Msumbiji tu ambayo imekumbwa na mafuriko hayo ambayo yalisababishwa na mvua kali upande wa kusini mwa Afrika na kujaza maji mito iliyokaribu na nchi hizo ikiwemo Zambia na Zimbabwe. Wakazi wanaoishi karibu na mto Zambezi wamekumbwa vibaya na mafuriko hayo na kusababishwa kuacha nyumba na mali zao.
Radio ya Msumbiji imesema mpaka sasa watu karibu 27,000 wanakabiliwa na uhaba wa chakula katika sehemu zilizokumbwa na mafuriko. Vilevile idara husika zimeonya kuwa kuna hatari ya maradhi makubwa kujitokeza kutokana na hali hiyo, maradhi hayo yakiwamo kuhara (diarrhoea) na malaria. Diarrhoea ni ugonjwa mkubwa Afrika ambao unauwa watoto na wakubwa.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||