![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Al Bangura aruhusiwa kuishi United Kingdom17/01/2008
Mcheza mpira wa miguu wa timu ya Watford, England, Al Bangura (19) ameruhusiwa kubaki nchini UK baada ya uamuzi wa idara ya mambo ya ndani (Home Office) kutangaza rasmi tarehe 14/01/2008. Al Bangura, ambaye amejaaliwa kupata mtoto mwezi uliopita, alihuzunika baada ya uamuzi wa mwanzo kabisa wa idara ya mambo ya ndani walipomkatalia maombi yake ya kuishi ya UK na kuombwa arudi nchini kwao Sierra Leone. Mashabiki wa timu ya Watford na mbunge wa mji huo Bibi Claire Ward, waliandaa kampeni ya kushawishi mamlaka wamruhusu Al Bangura kuishi UK. Kampeni hiyo ilisimamiwa na mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo Bwana Elton John na waziri wa mambo ya ndani wa zamani Bwana David Blunkett na kumuwezesha Al Bangura kuruhusiwa kuishi UK. Al Bangura alifika UK miaka minne iliyopita kwa kuomba ukimbizi nchini UK. Idara ya mambo ya ndani wamesema, kibali cha kufanya kazi na ruhusa hiyo iliyotolewa kwa Al Bangura, haimruhusu kuishi UK moja kwa moja, bali ni kwa kipindi cha muda wa makubaliano ya kimpira kati yake na timu ya Watford ambayo makubaliano yao yanakwisha mwaka 2010. Vilevile, Al Bangura ataangaliwa kiasi gani ataweza kuchangia katika kuleta maendeleo na ustadi wa mpira wa miguu wa England. Baada ya miaka hiyo, Al Bangura ataruhusiwa kuomba ruhusa ya kuishi moja kwa moja nchini United Kingdom.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||