![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
British Airways yaanguka Heathrow17/01/2008
Ndege ya abiria ya British Airways aina ya Boeing 777 namba (BA038), imeanguka kabla ya kufika katika uwanja wa ndege wa Heathrow, ilipojaribu kutua katika barabara yake ya ndege na kuseleleka kutoka kwenye majani mpaka kwenye lami ya barabara ya uwanja huo ilipokuwa ikitokea Beijing China.
Ajali hiyo ilitokea kwenye saa 6:42 mchana (GMT). Tairi za mbele za ndege hiyo zilivunjika hapo hapo baada ya kukita majani na kusababisha mabawa, injini na tumbo la ndege hiyo kuvunjika.
Abiria wote 36 na wafanyakazi wake 16 walisalimika na ajali hiyo na kutoka mara baada ya ndege hiyo kuanguka kwa kupitia kwenye maparachuti ya dharura. Watu sita walijeruhiwa na jeraha ndogo ndogo na walipata huduma ya kwanza hapo hapo uwanjani.
Gari za wagonjwa (ambulance) sita za uwanja wa ndege wa Heathrow na magari ya zima moto yote yalifika kwenye ajali hiyo.
Mmoja wa abiria, bwana Fernando Prada alisema, ajabu kuwa tulikuwa hatuna wasiwasi wowote wakati wa ajali hiyo na abiria wote tulitoka ndani ya ndege hiyo kwa dakika tu! Alisema, kupona kwenye ajali hii ni kama kushinda bahati nasibu. Waziri Mkuu Bwana Gordon Brown alikuwa kwenye ndege nyengine hapo hapo uwanja wa ndege wakati ndege hiyo inapata ajali.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||