Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Kevin Keegan arudi uwanjani

18/01/2008

Kevin Keegan alitambuliwa rasmi na washabiki wake kuwa ni meneja mpya wa timu ya Newcastle United tarehe 17/01/2008. Maongezi ya kumrudisha Kevin Keegan St. James Park, Newcastle, yalichukuwa masaa matatu mpaka kukubaliana kati ya timu ya Newcastle na Kevin Keegan.

Kevin Keegan (56), ambaye alikuwa ni mchezaji wa timu hiyo miaka ya 80 na kuwa meneja miaka ya 90, alipokewa kishujaa na mashabiki wake katika uwanja wa St. James Park kama meneja mpya wa Newcastle United.

Kevin Keegan aliwaambia waandishi wa habari kuwa kazi hii hainitishi kuichukuwa na timu hii hainitishi kuiongoza. Aliendelea kusema, washabiki wanataraji mengi katika timu hii, upinzani mkubwa ambao tunao ni vipi tutaweza kuwapatia wanayoyatarajia.

Meneja huyo mpya alisema, atajaribu kuongea na Alan Shearer, ambaye pia alikuwa ni mshambuliaji maarufu wa timu hiyo, kama atataka kufanya nae kazi katika kuindeleza timu hiyo, na kama atataka ataangalia nafasi gani Alan Shearer awe nayo katika kuiongoza timu hiyo.

Vilevile alisema, yupo tayari kufanya kazi pamoja na mshambuliaji maarufu Michael Owen ambaye katika kitabu chake alimsema meneja huyo kwa vibaya. Meneja huyo amesema kasikia yaliyoandikwa kuhusu yeye katika kitabu cha Michael Owen na ameridhia kwa kuwa ana haki ya kusema aonavyo na nipo tayari kufanya nae kazi.

Keegan, meneja mpya wa Newcastle, atatoka rasmi mbele ya washabiki wake na washabiki wa Newcastle kwenye mechi ya Newcastle na Bolton ambayo itachezwa Jumamosi jioni, tarehe 19/01/2008 katika uwanja wa St. James Park, Newcastle.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©