Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Mashujaa wa ndege ya British Airways (BA038)

18/01/2008

Peter Burkill (juu pichani) kapteni wa ndege ya British Airways namba BA038 iliyoanguka uwanja wa ndege wa Heathrow, London, wakati ilipokuwa ikitoka Beijing, China, adhuhuri ya tarehe 18/01/2008 alipokelewa kwa shangwe na wafanyakazi wa British Airways alipoingia katika ukumbi ambao alikutana na waandishi wa habari. Alisema kwa waandishi wa habari kuwa kutua salama kwa ndege hiyo ilikuwa ni moja ya ushirikiano kati yake na wafanyakazi waliyokuwa chini yake katika ndege hiyo.

Kapteni huyo ambaye ni baba wa watoto watatu, alimsifu msaidizi wake bwana John Coward kwa ustadi alioutumia katika kusaidiana kuileta ndege ya aina ya Boeing 777 uwanjani. Hapo hapo akawasifu wahudumu wa abiria wa ndege hiyo kufanya kazi nzuri ya kuwatoa abiria kwenye ndege hiyo kiweledi.

Mkurugenzi wa wafanyakazi wa huduma za ndani ya ndege (pichani kulia) Sharon Eaton-Mercer, pia aliwasifu wafanyakazi wake kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Katika hotuba yake fupi, kapteni huyo hakuzungumzia kwanini ndege hiyo ilianguka.

Ripoti ya wachunguzi wa ajali za hewa walisema, ndege hiyo ilipofika futi mia sita (600 feet) kutoka usawa wa dunia na ubali wa maili mbili (2 miles) kufikia kwenye barabara yake, injini mbili za ndege hiyo zilishindwa kusukuma uzito wa ndege hiyo kufikia barabara yake na kusababisha kutua kwenye kwa mshindo mkubwa kwenye majani kabla ya barabara ya ndege.

Ripoti hiyo ni ripoti ya mwanzo na uchunguzi wa ndege hiyo na wachunguzi wa ajali za hewa bado unaendelea kwa kutaka kujua vipi ndege ya kileo kama hiyo ambayo imeundwa na shirika kubwa la ndege kama Boeing ambayo ina historia nzuri ya usalama kuweza kuanguka.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©