Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Batman na Robin wa Argos

19/01/2008

Kamera ya Zenjydar imemnasa Batman na Robin ambao walikuwa wakichangamsha watu na huku wakigawa toleo jipya la vitabu (catalogues) vya duka la Argos ambalo lipo maeneo ya Beckton, mjini London. Argos ni moja kati ya maduka makubwa ya nchini UK ambayo yanauza bidhaa tofauti za mahitaji ya kila siku.

Batman na Robin wametokea kupendwa na watoto kutokana na vitabu vyake vya katuni ambayo inagusia watu hao wawili (Batman na Robin) na kuja kupendwa na watu wazima baada ya kitabu hicho kufanywa kuwa filamu.

Chanzo cha Batman na Robin kama kinavyozungumziwa na mtunzi wa vitabu hivyo, ni Bruce Wayne ambaye ni (Batman) alishuhudia mauaji ya wazazi wake walipokuwa wakiuliwa mbele yake na baadaye kuamua kujiita Batman na kupigana vita na jinai. Na baada ya Dick Grayson ambaye ni (Robin) walipouliwa wazazi wake, Batman alimchukuwa na kumfundisha ustadi wa kupigana vita na jinai.

Filamu ya mwisho ya Batman ilitoka mwaka 2005 - Batman Begins. Hollywood (db Techno) Warner Bros. wameshatengeneza filamu mpya ya Batman ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni, lakini imecheleweshwa kutokana na mabishano na waandishi wa Hollywood ambayo yametokea wiki zilizopita.

Filamu hiyo inaitwa Justice League ambayo muendeshaji filamu hiyo aliitaka iwe katika majumba ya sinema mwanzoni mwa mwaka 2009, lakini kuna uwezekano wa kuchelewa mpaka mwaka 2010 pamoja na filamu mpya ya Superman ambayo ipo matayarishoni.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©