![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Umoja wa nchi za Ulaya wataka utulivu Kenya20/01/2008
Baada ya mazungumzo na rais wa Ghana na baada ya mazungumzo na bwana Koffi Annan kushindikana kuhusu vurugu la Kenya, kamati maalum ya nchi za umoja wa ulaya (EU) wamewasili nchini Kenya kuleta utulivu nchini humo. Wamesisitiza kwa pande zote mbili za upinzani kusimamisha uchochezi ambao umesababisha vifo na chuki kati ya wananchi nchini Kenya. Bwana Louis Michel ambaye anaongoza kamati hiyo ameshawasili nchini Kenya na mpaka sasa ameshaongea na viongozi wa pande zote mbili za upinzani, rais Mwai Kibaki na mpinzani wake wa chama cha ODM, Raila Odinga.
Katika mkutano huo ambao ulifanyika mjini Nairobi na viongozi wa vyama vyote viwili, bwana Louis Michel aliwaomba vyama vyote viwili kuwashauri polisi wa Kenya kupunguza nguvu ambazo wanazitumia kwa raia wanaoshabikia upinzani na akaongeza kwa kusema, tunaomba utulivu na utulivu uwe wa manufaa ya kuleta maelewano. Hapo hapo alikiomba chama cha upinzani kupunguza maandamano ya mara kwa mara ambayo huwa yanaelekea kwenye vurugu na vifo. Bwana Koffi Annan anatarajiwa kurudi tena Kenya na kuwepo kwenye mazungumzo hayo ya kuleta utulivu nchini humo.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||