![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
David Beckham atembelea Afrika22/01/2008
Mchezaji mpira maarufu duniani, David Beckham, atembelea Sierra Leone katika ziara yake ya siku nne kama balozi wa UNICEF katika kampeni ya kusaidia magonjwa ya watoto katika nchi zinazoendelea. Alitumia muda wake kudhihaki na watoto kama aonekanavyo pichani juu akiwa na Senyo, mtoto mwenye umri wa miaka mitano.
Vilevile alitembelea watoto wachanga na baadaye kujifurahisha na vijana wa mjini kwa kuomba namba kucheza nao mpira wa miguu ambao uliandaliwa mechi ya timu ndogo mbili za hapo hapo Freetown.
Alitangazia dunia katika ziara yake na kusema, tusifunge macho kwa watoto wanaokufa duniani katika nchi zinazoendelea kwa maradhi yanayoweza kuzuilika. Na baada ya hapo alitembelea katika vituo mbalimbali vya watoto huko Freetown, Sierra Leone.
Katika mechi hiyo, alichukuwa muda kuwafundisha watoto kupiga mpira kama anavyoupiga yeye kwa umaarufu wake wa 'bend it like Beckham'.
Mkurugenzi mkuu wa Unicef UK, bwana David Bull, alimpongeza David Beckham kutembelea Afrika na kuonyesha kuwa kuna mahitaji ya watoto wa Afrika kuangaliwa katika afya zao.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||