Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Virgin Atlantic yazindua dizaini ya 'Spaceliner'

23/01/2008

Virgin Galactic ya (Virgin Atlantic) wamezindua dizaini ya ndege ambayo itakayochukuwa abiria kwenda angani kwa matembezi ya utalii. Mwenye kumiliki shirika la ndege hilo bwana Richard Branson, alisema kutangazia waandishi wa habari mjini New York kuwa, ndege hiyo ambayo inategemewa kuanza huduma zake mwaka 2009 (mwakani), itakuwa na ushindani mkubwa katika uekezaji ambao utashinda uekezaji wa simu za mikono na teknolojia ya mtandao ambazo mwanzoni zilikuwa zikitumika jeshini na baadaye kutumika kwa watu binafsi.

Virgin Galactic iliingia mkataba na msanifu maarufu kwa ubunifu wa miundo ya mambo ya anga, bwana Burt Rutan kutengeneza miundo ya ndege za Virgin Galactic, ambazo zitakazochukuwa abiria wa kwenda angani kwa utalii.

Ndege hiyo, itabebwa na ndege nyengine ambayo inajulikana kama (White Knight Two) ambayo itakwenda mpaka itakapofikia kikomo chake itabana mabawa yake na kuiachia ndege itakayobeba abiria (Spaceliner) kufungua mabawa yake na kuongoza kuelekea kituoni.

Ndege hiyo itaanza mazoezi yake miezi ijayo ya mwaka huu (2008), ina uwezo wa kubeba marubani wawili na abiria sita. Uwanja wa ndege wake upo katika jangwa la New Mexico, America, ambao unaitwa (Spaceport America).

Tikiti ya ndege hiyo kwa kila abiria ni $200,000 (dola laki mbili za Kimarekani) na mpaka sasa watu 200 wameshaagiza tiketi zao na wengine 85,000 wamejisajili kwa tiketi za baadaye.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©