Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Filamu mpya ya James Bond kuitwa 'Quantum of Solace'

24/01/2008

Imezinduliwa rasmi kuwa filamu mpya ya 007 James Bond kuitwa 'Quantum of Solace'. Jina hilo limechukuliwa kutoka kwenye kitabu cha mtunzi wa hadithi za vitabu vya 007 katika miaka ya 60 bwana Ian Fleming. Filamu hiyo imeanza kuchukuliwa tangu mwezi Novemba, 2007.

Mtoaji wa filamu hiyo bwana Michael Wilson alisema, filamu hii itakuwa na undundu kuliko filamu ya James Bond iliyotolewa mwaka 2006 Casino Royale. Daniel Craig pichani juu, alikuwa ndiyo nyota wa filamu ya Casino Royale na pia ndiyo atakayekuwa nyota wa filamu hii mpya Quantum of Solace.

Waandishi wa habari walitembelea majengo yanayofanyiwa filamu hiyo na walipata fursa ya kuonyeshwa kipande cha dakika moja cha filamu hiyo kinachoonyesha 007 James Bond akining'inia kwenye kamba baada ya mripuko mkubwa wa moto kwenye nyumba ya sanaa iliyopo Siena, Italy. Kipande kingine walionyeshwa 007 James Bond (Daniel Craig) akikutana kimazungumzo na 'M' (Judi Dench) nje kwenye theluji.

Pichani kushoto ni Olga Kurylenko, ambaye anacheza kama mpenzi wa James Bond kwenye filamu ya Quantum of Solace, akijulikana kwa jina la Camille, na kulia pichani ni Gemma Arterton, ambaye anacheza kama muwakilishi wa MI6. Filamu ya Quantum of Solace inategemewa kuwa kwenye majumba ya sinema, Novemba, 2008.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©