![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Reli ya Tanzania na Rwanda kuanza mwakani25/01/2008
Rais wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akizungumza na Bw. Daniel Cooper (pili kushoto) na Bw. Tom Veegh (kushoto), ambao ni sehemu ya ujumbe wa Barlington Northern Santa Fe (BNSF) ambapo walizungumzia juu ya suala la ujenzi wa reli kuanzia Isaka (Tanzania) hadi Kigali (Rwanda), Ikulu, Dar es Salaam. HABARI KAMILI: Ujenzi wa reli kuunganisha Isaka, Tanzania na mji mkuu wa Rwanda, Kigali umepangwa kuanza mwakani, Rais Jakaya Kikwete ameambiwa leo. Ujumbe wa kampuni ya Barlington Northern Santa Fe (BNSF) kutoka Marekani pia umemwambia Rais Kikwete kuwa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika 2013. Ujumbe huo pia umemwambia Rais kuwa kazi ya ujenzi wa reli hiyo mpya, utakwenda sambamba na matengenezo makubwa na upanuzi wa Reli ya Kati, kati ya Isaka na Dar es Salaam. Upanuzi huo utalenga kuiwezesha Reli ya Kati kufikia kiwango cha kimataifa cha reli, kuongeza nguvu ya reli hiyo kuweza kubeba mabehewa zaidi, na kubeba mizigo mikubwa zaidi na kupunguza muda wa safari. Katika mazungumzo kati ya ujumbe huo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam, ujumbe huo pia umemwambia kuwa mahitaji yote muhimu kwa ajili ya ujenzi wa reli kati ya Isaka na Kigali karibu yanakamilika. Ujumbe huo ulikuwa ni pamoja na Daniel Cooper na mashirika wake, Tom Veegh kutoka kampuni ya masuala ya fedha ya Fox River Financial Resources, ambayo inahusika na masuala ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo, pamoja na John Orrison kutoka kampuni ya BNFS. Mazungumzo hayo pia yamehudhuriwa na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji; Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge na Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Dk. Juma Ngasongwa. Wakati maandalizi yanaendelea kwa ajili ya ujenzi wa reli ya Isaka-Kigali, na upanuzi wa Reli ya Kati, maandalizi pia yanafanyika kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa ujenzi wa reli kati ya Isaka-Kigali-Bujumbura. Mbali na hiyo, mipango pia inaandaliwa na kuangalia uwezekano wa kuunganisha Isaka na mji wa Mwanza, na kuunganisha Tabora na Kigoma kwa reli bora zaidi. Rais ameuelezea ujumbe huo kuhusu furaha yake kusikia habari hizo, na kusema kuwa Serikali yake inaiunga mkono mipango hiyo kwa “asilimia 150”. “Ujumbe wangu ni mfupi tu – tunataka njia ya reli. Na tunaunga mkono juhudi zenu asilimia 150,” Rais ameuambia ujumbe huo. Rais pia ametaka kuangaliwa kwa uwezekano wa kuunganisha Reli ya Kati na Reli ya TAZARA, na hivyo kuwezesha mizigo kutoka kusini mwa Afrika kusafirishwa hadi Tanzania, na mizigo ya majirani wa kaskazini wa Tanzania kusafirishwa kwa urahisi kwenda kusini mwa Afrika. Ameuambia ujumbe huo kuwa upanuzi na matengenezo makubwa katika Reli ya Kati utakwenda sambamba na upanuzi mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam. Ikulu, Dar es Salaam - 25 Januari, 2008
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||