![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Aina ya pesa za utalii wa Anga 'QUID'26/01/2008
Wanasayansi wamezindua pesa zitakazotumika kwenye matumizi ya kila siku kwenye utalii wa anga ambao baadhi ya mashirika wameekeza katika maeneo hayo ya utalii wa anga likiwemo shirika la Virgin Galactic ambalo linamilikiwa na Bw. Richard Branson wa Virgin Atlantic. Pesa hizo zinaitwa 'Quasi Universal Intergalactic Denomination' au QUID. Pesa hizo ambazo hazina aina yoyote ya madawa na hazina pembe kali, zimesanifiwa na Wanasayansi (wa kutoka kituo cha anga na Wanasayansi wa kutoka chuo kikuu cha Leicester) kuhimili hali ya hewa ya anga na vilevile kwa usalama wa watalii. Profesa George Fraser wa chuo kikuu cha Leicester alisema, hakuna pesa zozote au kadi zozote ambazo tunatumia hapa duniani zinaweza kutumika angani.
Wanasayansi wa kituo cha anga wamesema, miaka mitano ijayo utalii wa kwenda angani utakuwa ni kitu cha kawaida; na wanatarajia mwaka 2050 kutakuwa karibu na vitu vyote ambavyo vipo duniani vitakuwa mwezini na kutakuwa ni sehemu kubwa ya utalii. Itakapofikia hivyo, kutakuwa na biashara kubwa kati ya mwezini na duniani na kwahivyo, Profesa George amesema, kutakuwa na biashara kubwa ya ubadilishaji wa pesa za angani hapa duniani. Kampuni ya ubadilishaji wa pesa Travelex au (Travel Exchange) ambao wameshirikiana na Wanasayansi hao katika uundaji wa pesa hizo wamesema, biashara ya kwenda angani ikishamiri, hatutoona ajabu watu wakiingia katika maduka yetu na kuomba kubadilisha pesa za kukaa hoteli kwa wiki mbiili angani.
Mpaka sasa pesa hizo zinathamani ya 1Quid = £6.25
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||