Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Hali ya hewa ya China yaathiri usafiri

30/01/2008

Maelfu ya watu wamekwama kwenye vituo vya treni na viwanja vya ndege kwasababu ya hali mbaya ya hewa iliyochafuka nchini China. Hali kama hiyo haijawahi kutokea kwa miaka mingi iliyopita kama walivyotangaza vyombo vya habari vya China.

Mwaka mpya wa Kichina ukikaribia, maelfu ya watu hao ambao wengi wao wametokea mikoa ya mbali wanajaribu kupigana vita na usafiri ili wawe nyumbani kwa mwaka mpya na familia zao.

Hali hiyo mbaya ya hewa ambayo imesababishwa na theluji kubwa iliyoshuka nchini China ambayo imesababisha mtandao wa usafiri kuathiri misafara ya wananchi.

Serikali ya China imeamrisha maelfu ya maaskari wake kusambaza mablanketi na vyakula kwenye vituo vya usafiri. Hapo hapo, serikali wamesambaza maelfu ya barua ambazo zinawasihi wananchi kughairi safari zao na kubakia walipotoka ili kuepukana machafuko ya usafiri.

Kwa wengine, mwaka mpya wa Kichina ndiyo muda pekee wa kwenda kuona familia zao baada ya kazi na kusevu pesa zao kwa miezi. Baadhi yao hawakukata tamaa na kuendelea na kutafuta njia tofauti ya usafiri kuelekea nyumbani.

Kwa wale waliofanikiwa kupata usafiri, walikuwa na bashasha lakini kurudi kwao hakutarajiwi mapema mpaka barabara za usafiri zirudi kwenye hali yake ya kawaida.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©