![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Je, David Beckham aachwa kwenye mataa?31/01/2008
David Beckham ameachwa katika kundi la mwanzo la wachezaji wa timu ya taifa ya England na meneja mpya wa timu hiyo Fabio Capello. Lakini meneja huyo hajaufunga mlango wake moja kwa moja kwa David Beckham, ila alisema, pia ana wasiwasi kwa sasa David hayuko fiti kuchezea timu ya taifa na hasa ikiwa timu hiyo inakabiliana na mechi na Switzerland mwezi ujao tarehe 06/02/2008, Jumatano. Vilevile, Golikipa Paul Robinson ameachwa kwenye mataa na hatochezea timu ya taifa. Hapo hapo, mchezaji wa Aston Villa Cartis Davies na Gabriel Agbonlahor wamechaguliwa katika mkupuo wa kwanza wa timu ya taifa. Capello amesema, sababu ya kuwa hajamchagua Beckham katika kikundi hiki cha mwanzo ni kuwa, tangu mechi yake ya mwisho kucheza na Croatia Novemba mwaka jana, hajacheza mechi yoyote kubwa ya kiushindani wa kimataifa. Aliongezea kusema, aliongea na David Beckham kwenye simu na alimshauri kuwa si kama kamuacha moja kwa moja katika timu ya taifa na atamuangalia maendeleo yake katika mechi zake zijazo atakazochezea akiwa Marekani na timu yake ya L.A. Galaxy. Hapo hapo, Beckham alivyohojiwa na vyombo vya habari alipokuwa katika ziara yake Jumanne iliyopita nchini Brazil, alisema yuko fiti kiafya na kimpira na yuko tayari kuchaguliwa katika timu ya taifa. Beckham aliwahi kuwa pamoja na Fabio Capello alipokuwa akichezea Real Madrid ya Spain na Capello kama meneja wa timu hiyo, Je, Beckham atachezea tena timu ya taifa ya England?
Capello atamalizia uamuzi wake wa kuchagua wachezaji wa timu ya taifa ya England Jumamosi ijayo ya tarehe 02/02/2008, na vilevile ataamua nani kuwa kapteni wa timu ya England wakati kapteni John Terry aliyechaguliwa na meneja aliyepita (Steve McClaren) pia kaachwa kwenye mataa kwasababu ya kuumwa kwake kwa mguu. Wachezaji wa timu ya taifa watakaocheza Switzerland wiki ijayo tarehe 06/02/2008: Goli-kipa: David James (Portsmouth), Scott Carson (Liverpool on loan at Aston Villa), Chris Kirkland (Wigan) Wahami: Wayne Bridge (Chelsea), Ashley Cole (Chelsea), Curtis Davies (West Brom on loan at Aston Villa), Rio Ferdinand (Manchester United), Glen Johnson (Portsmouth), Ledley King (Tottenham Hotspur), Nicky Shorey (Reading), Wes Brown (Manchester United), Joleon Lescott (Everton), Micah Richards (Manchester City), Matthew Upson (West Ham United), Jonathan Woodgate (Tottenham Hotspur) Viungo: Michael Carrick (Manchester United), Steven Gerrard (Liverpool), Gareth Barry (Aston Villa), Jermaine Jenas (Tottenham Hotspur), Owen Hargreaves (Manchester United), Joe Cole (Chelsea), Ashley Young (Aston Villa), Stewart Downing (Middlesbrough), Shaun Wright-Phillips (Chelsea), David Bentley (Blackburn Rovers) Washambuliaji: Emile Heskey (Wigan Athletic), Gabriel Agbonlahor (Aston Villa), Michael Owen (Newcastle United), Wayne Rooney (Manchester United), Peter Crouch (Liverpool)
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||