![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Rais JK amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika31/01/2008
JK akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe wakiwa katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika (AU) jana Mjini Addis Ababa, Ethiopia, leo muda mfupi kabla JK hajachaguliwa kuwa mwenyekiti wa AU. Habari kamili soma chini. Rais Jakaya Kikwete amechaguliwa kwa kauli moja na wakuu wa Umoja wa Afrika (AU) kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja huo kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao. Baada tu ya kukabidhiwa wadhifa huo, Rais Kikwete alisema kazi kubwa ya umoja huo ni kuhakikisha inaondokana na jinamizi la kuonekana kazi yake kubwa ni kushughulikia migogoro ya kisiasa badala ya maendeleo. Wakati wakuu wa nchi hizo walipokutana jioni baada ya mapumziko ya mchana mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Rais John Kufour wa Ghana, alimwita Balozi wa Misri katika Umoja huo, Balozi Khalid na kumtaka kutangaza matokeo ya uchaguzi huo. Balozi Khalid kwa lugha ya Kiarabu, alisema baada ya mashauriano na mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao katika umoja huo, wamekubaliana kwa kauli moja kuwa Mwenyekiti wa Umoja huo atakuwa Tanzania, kwa maana ya Rais Kikwete; kisha akatangaza wasaidizi wake kuwa watatoka Libya, Lesotho na Cameroon kwa mgawanyo wa kikanda, yaani Kaskazini, Kusini na Kati. Baada ya hapo, Rais Kufour alimwita kwenye meza kuu Rais Kikwete ambaye aliondoka kwenye kiti chake alichokuwa amekaa na kwenda meza kuu kuungana na viongozi wengine, kabla ya Rais wa Ghana kumkabidhi kirungu kama ishara ya uenyekiti huo. Nchi nyingine zilizowahi kuwa Mwenyekiti wa AU tangu ilipoanzishwa mwaka 2002 ni Afrika Kusini (Julai 2002 hadi Julai 2003), Msumbiji (Julai 2003 hadi Julai 2004), Nigeria (Julai 2004 hadi Januari 2006), na Congo Brazzaville. Rais Kikwete aliyeingia ukumbini jioni akiongoza wakuu wengine wa nchi akifuatana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika, Alpha Oumar Konare, akizungumza kwa lugha ya Kiswahili baada ya kukabidhiwa madaraka hayo, alisema anaipokea nafasi hiyo kwa unyenyekevu na akaomba ushirikiano kwa wakuu wenzake wa nchi ili kuiletea Afrika maendeleo.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||