![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Kikwete akemea siasa za chuki04/02/2008
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete amewataka wananchi wa kisiwani Pemba, kuacha siasa za chuki na kuthamini maendeleo makubwa yaliyopelekwa na Serikali. Akihutubia wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 31 tangu kuzaliwa kwa CCM, Rais Kikwete alisema Pemba imepata mafanikio makubwa katika sekta za barabara, maji safi na salama na umeme. Alisema barabara nyingi zimejengwa kisiwani humo zikiwemo za Mtuhaliwa-Chake, Chakechake ``Mkoani, Wesha Chakecheke na nyingine zipo katika mpango wa matengenezo kwa kushirikiana na wafadhili. Alisema barabara hizo zinazojengwa zina urefu wa kilomita 123, ikiwemo ya Mzambarautakao ``Finya, Kuuyu Kangagani na Kojani Wete-Gando. Alisema hivi sasa serikali ya Zanzibar imefanikiwa kutengeneza bandari za Wete na Mkoani ambazo zitatoa mchango mkubwa katika kukuza kipato cha wananchi na serikali. Aliongeza kuwa, hivi sasa mradi mkubwa wa umeme kutoka Tanga hadi Pemba kupitia chini ya bahari, unaendelea kutekelezwa na kukamilika kwake kutamaliza tatizo sugu la uhaba wa huduma ya umeme kisiwani humu. "Tuachane na watu wanaoeneza chuki, pale penye mafanikio, lazima tuseme kweli hata kama hatupendi," alisema. Kuhusu mazungumzo ya kumaliza mpasuko wa kisiasa kati ya CCM na CUF, alisema dalili zinaonyesha yatafanikiwa. Alisema jambo la msingi ni wana-CCM na CUF, kuwa na subira wakati viongozi wakiendelea kukamilisha hatua za mwisho za mazungumzo hayo. Hata hivyo, alisema CCM sio chanzo cha tatizo lililopo na ndio maana ilikuwa ya kwanza kuamua kukaa pamoja kutafuta ufumbuzi wake. Rais Kikwete alisema lengo kubwa la mazungumzo hayo ni kubadilisha mahusiano na kuondoa uadui na siasa za uhasama na badala yake kujenga misingi bora ya demokrasia. Aliwakumbusha viongozi wa CCM kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama ili kujenga mazingira mazuri ya ushindi mwaka 2010. Alisema serikali inakusudia kuimarisha uwajibikaji na kuwataka viongozi kuzingatia umuhimu wa maadili ya uongozi na kupiga vita vitendo vya rushwa. Katika maadhimisho hayo, wanachama 1,000 kutoka mikoa miwili ya Pemba, walipewa kadi za CCM. Alisema CCM itaendela kuimarika kwa kuwa na viongozi waadilifu na wajasiri. Mapema, akimkaribisha, Rais Kikwete, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar, aliwataka wapinzani wakae chonjo katika uchaguzi wa mwaka 2010 kwa kuwa CCM ina nafasi kubwa kuchukua viti kisiwani Pemba. Alisema kwamba ni kweli katika uchaguzi uliopita, CCM haikufanikiwa kupata kiti kisiwani huko, lakini mahudhurio yaliyoonyeshwa na wananchi katika mkutano huo, ni dalili za ushindi wa chama hicho. Viongozi mbalimbali walihudhuria sherehe hizo wakiwemo Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein, Waziri Kiongozi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha, Naibu Waziri Kiongozi, Bw. Ali Juma Shamuhuna na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Saleh Ramadhan Ferouz.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||