Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Steven Gerrard - Kapteni wa timu ya England

05/02/2008

Meneja wa timu ya taifa ya England, Fabio Capello, ametangaza rasmi kuwa Steven Gerrard atakuwa kapteni wa timu ya taifa ya England katika mechi inayowakabili ya Jumatano ya tarehe 06/02/2008 wakicheza na Switzerland. Steven Gerrard ni kapteni wa timu ya Liverpool kabla ya kuteuliwa kuwa kapteni wa England na mechi hii itakuwa ndio mechi yake ya kwanza kuwa kama kapteni wa timu yake ya taifa (England).

Capello alimsifia Gerrard kwa jitihada zake za kimpira, lakini hapo hapo alisema nafasi hiyo ya ukepteni utakuwa ni wa muda mfupi mpaka atakapotaja kapteni wa moja kwa moja itakapofikia karibu na mechi na Andorra itakayochezwa Septemba 6, katika kugombea nafasi ya kwenda Afrika ya kusini kwenye kombe la dunia ambayo itakuwa mwaka 2010. Mpaka wakati huo, Capello atakuwa na muda wa kutosha kuangalia makapteni tofauti katika timu yake.

Capello alisema, uamuzi huo aliwazungumzia wachezaji wake kwanza kabla ya kutangaza kwenye vyombo vya habari. Na aliongeza atawajulisha wachezaji wote nani ambaye atakayecheza siku hiyo na Switzerland kabla ya kutoka hotelini kuelekea kwenye mechi.

Alipoulizwa kuhusu kutomchagua David Beckham, alisema, tuzungumze kuhusu wachezaji watakaocheza kwenye mechi ijayo siyo ambao hawatocheza.

Inavyosemekana Capello kawakataza wachezaji kutumia simu na vilevile kaamua kuwaita wachezaji hao kwa majina yao ya ukoo badala ya majina yao ya kwanza. Capello amesema, nimeweka masharti kwa wachezaji na kawaomba masharti hayo yasivunjwe. Kwa mfano, watakula pamoja mezani na wataondoka pamoja, alisema hiyo itaonyesha ishara ya kuheshimiana na vilevile kufika kwa wakati.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©