Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

England 2 - 1 Switzerland = CAPELLO

06/02/2008

England 2, Switzerland 1. Goli la kwanza la England limefungwa na Jermaine Jenas katika dakika ya 40, na goli la pili limefungwa na Shaun Wright-phillips katika dakika ya 62.

Fabio Capello kashinda mechi yake ya kwanza, lakini je, mashabiki wa timu ya England wajisahau na ushindi huo mmoja?

Kihistoria, Meneja sita waliopita waliyoongoza timu ya England katika mechi zao za kwanza walishinda akiwemo Graham Taylor, ambaye alishindwa kuipeleka England kushindana World Cup ya mwaka 1994 iliyofanyika Marekani.

Wakati utamu wa ushindi haujaisha na wachezaji kuonyesha machejo na ari uwanjani kwa pasi na kuonana, bado kazi ipo mbele hasa katika kulikimbilia kombe la dunia ambayo michuano yake inaanza mwezi wa tisa mwaka huu.

Steven Gerrard alionyesha maana ya kuwa Kapteni na aliitumia nafasi yake kwa ari na kuonyesha mfano mzuri akiwa kama ni nahodha wa wachezaji wake.

Kabla ya michuano ya mwezi wa tisa ya kugombea nafasi ya kwenda Afrika ya kusini mwaka 2010, Capello na kundi lake watarudi tena uwanjani inasemekana mwezi wa tano katika mechi ya kirafiki ya majaribio ya timu yake kwenda Afrika kusini.

Na kabla ya mechi hiyo, Wana wa Capello watacheza na France mjini Paris, tarehe 26/03/2008, na kabla ya hapo kunradhi wapenzi wa Uswizi, England na Capello itakuwa ndiyo mechi yao ya kwanza ya kisawasawa kuonyesha nguvu yao mpya chini ya Meneja wao mpya Capello.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©