JK atangaza baraza jipya
la Mawaziri
12/02/2008

Rais wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete aliingia katika ukumbi wa Tamisemi, Dodoma, saa tisa na dakika
kumi na sita akiongozana na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na
Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda.
Katika kuanza alitoa maelezo na alisema
kwamba wamezingatia kazi mbili katika kuamua.
-
Kwanza, kutazama muundo wa serikali
-
Pili, kujaza nafasi za kujaza
baraza la Mawaziri
KABLA HAJATANGAZA BARAZA LA
MAWAZIRI,RAIS JK AMESEMA VIONGOZI WA MUDA MREFU WAMEOMBA KUPUMZIKA AMBAO
NI:
1. JOSEPH MUNGAI
2. KINGUNGE NGOMBALE MWIRU
BARAZA LENYEWE NI:
1. WAZIRI OFISI YA RAIS (UTAWALA BORA) SOFIA SIMBA
2. WAZIRI OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UMMA) HAWA GHASIA
3. WIZARA OFISI YA MAKAMU WA RAIS (SHUGHULI ZA MUUNGANO) MOHAMED SEIF
KHATIB
4. WIZARA YA UTALII NA MAZINGIRA DK. BATILDA BURIANI
5. WAZIRI OFISI YA MAKAMU WA RAIS (SERA NA URATIBU WA BUNGE) PHILIP
MARMO
6. WIZARA YA TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA STEVEN WASIRA
7. WIZARA YA FEDHA MUSTAFA MKURO NA MANAIBU NI JEREMIAH SUMARI NA OMARI
YUSUF MZEE
8. WIZARA YA AFYA PROFESA DAVID MWAKYUSA NAIBU NI AISHA KIGODA
9. WIZARA YA ARDHI JOHN CHILIGATI
10. ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI PROFESA JUMANNE MAGHEMBE NAIBU GAUDENSIA
KABAKA NAIBU NI MWANTUMU MAHIZA
11. WIZARA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA SHUKURU KAWAMBA NAIBU NI DK. MAUA
DAFTRI
12. WIZARA YA MIUNDO MBINU ANDREW CHENGE NAIBU DK. MAKONGORO MAHANGA
14. WIZARA YA UTAMADUNI NA MICHEZO GEORGE MKUCHIKA NAIBU JOEL BENDERA
15. WIZARA YA KAZI NA AJIRA POFESA JUMA KAPUYA NAIBU HEZEKIA CHIBULUNJE
16. WIZARA YA MAJI PROFESA MARK MWANDOSYA NAIBU CHIZA
17. WIZARA YA KILIMO NA CHAKULA MATHAYO DAVID MATHAYO
18. WIZARA YA MENDELO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO MARGARETH SITTA NAIBU
NI LUCY NKYA
19. WIZARA YA UVUVI NA MIFUGO JOHN POMBE MAGHUFULI NA MANAIBU NI
SHAMSA MWANGUGA NA EZEKIEL MAIGE
20. WIZARA YA MAMBO YA NDANI LAWRENCE MASHA NAIBU NI HAMISI KAGASHEKI
21. WIZARA YA MAMBO YA NJE NI BERNARD MEMBE NAIBU SEIF ALI IDDI
22. WIZARA YA NISHATI NA MADINI WILLIAM NGELEJA NAIBU ADAM MALIMA
23. WIZARA YA SHERIA MH. CHIKAWE
24. WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DK. HUSSEIN MWINYI NAIBU
DK EMMANUEL NCHIMBI
25. WIZARA YA AFRIKA MASHARIKI DK. E. KAMALA
26. WIZARA YA VIWANDA NA BISHARA DK. MARY NAGU NAIBU CYRIL CHAMI

Aliyekua Waziri ofisi ya Rais na mshauri
mkuu wa rais katika maswala ya siasa Mh. Kingunge Ngombale Mwiru (Pichani
juu) ameomba kupumzika katika nyadhifa hiyo baada ya kulitumikia taifa
kwa muda mrefu,kiongozi mwingine aliyeomba kumpumzika ni Mh. Joseph
Mungai.
Aidha Rais Jakaya Kikwete katika kutangaza
baraza jipya la mawaziri leo hii mjini Dodoma ndani ya ukumbi wa
Tamisemi, kwenye uteuzi huo amewaacha Mawaziri kadhaa akiwemo Bi Zakia
Meghji, Dan Nsanzugwanko, Rita Mlaki, Basil Mramba, Juma Ngasongwa,
Bakari Mwapachu, Prof. Msolwa, Zubeid Mhita, pamoja na Antony Diallo.

|