Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Tawi la CCM London lampongeza Rais JK

14/02/2008

Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Uingereza kimempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa uteuzi wa Wazir Mkuu Mpya, Mheshimiwa Bw. Mizengo Pinda na kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti mpya wa umoja wa nchi za Afrika (OAU).

Hayo yalisemwa na mgeni rassmi wa shughuli hiyo na ndio mlezi na muhasisi wa tawi la CCM London, Bw. Sharif Maajar wakati wa sherehe za kusheherekea kwa CCM kutimiza miaka 31 zilizofanyika Reading na kuhudhuriwa na halaiki ya wanachama wa CCM na kiongozi Balozi wa Tanzania, Bi Mwanaidi Maajar aliyemsindikiza mumewe.

Bw. Maajar alisema Rais Kikwete ametumia hekima zake kumteua Mheshimiwa Pinda kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuridhia uamuzi wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu baada ya kuhusishwa katika kashfa ya mkataba wenye utata wa Richmond.

“Kweli ni mwana CCM mwenzetu ni mtu mwadilifu wa kusimamia haki, kwa hili sote tumefarijika sana. Tunampongeza Rais Kikwete na sisi wa huku ughaibuni tutampatia ushirikiano wa kutosha,” alisema.

Bw. Maajar alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Kikwete kwa kuteuliwa kwake kuwa mwenyekiti mpya wa OAU, hatua ambayo imetokana na uongozi wake shupavu, hali iliyofanya viongozi wenzake wa Afrika kumkabidhi kijiti cha uongozi wa OAU.

Mlezi huyo wa CCM London alisema Mheshimiwa Rais ameonesha kukubalika kwake hata na mataifa ya nje, hivyo kuna kila sababu ya wana CCM na Watanzania kwa ujumla kujivunia mafanikio makubwa ambayo Tanzania inayapata kupitia kwa Rais Kikwete.

“Kweli ameipatia heshma kubwa sana Tanzania na Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivyo nawaomba wana CCM wenzangu tuendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika juhudi zake za kuleta amani Afrika na maendeleo ya Tanzania,” alisema Bw. Maajar.

Awali mwenyekiti wa CCM London, Bw. Maina Owino alisema tawi lake la Uingereza linaandaa mikakati mikubwa ambayo itatakayokuwa na faida kwa CCM Taifa ikiwemo kuwaanda wana siasa wachanga ambao wako masomoni huku Ulaya ili waweze kukiendeleza chama.

“Kazi kubwa ambayo sisi kama chama ni kuwashawishi vijana kujiunga na chama ili warudipo nyumbani waweze kukijenga na kukiimarisha chama, hivyo tutajitahidi kadri tuwezavyo kulifanikisha hili,” alisema Bw. Owino.

Pia alitumia nafasi hiyo kuwapa pole raia wa Kenya ambao walialikwa katika sherehe hizo kwa matatizo ya kisiasa yaliyotokea nchini na kusababisha mauaji ya halaiki kubwa ya watu wasiokuwa na hatia na kuomba kuwa 'a subway' wakati suluhisho la amani linatafutwa chini ya msimamizi, Koffi Anan.

“Tunawaomba wenzetu kuwa na subira katika wakati huu mgumu kule nyumbani Kenya, lakini tunaamini matatizo ya huko yataisha na Kenya yetu kurudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Bw. Owino.

Na Juma Pinto, London

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©