Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Rais George Bush asaini miradi ya maendeleo

17/02/2008

Baadhi ya akina mama wakimlaki kwa vifijo na nderemo Rais wa Marekani George W. Bush leo asubuhi ndani ya viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na mgeni wake, Rasi George Bush leo asubuhi Ikulu.

JK na mgeni wake Rais George W. Bush leo ikulu wameweka saini mkataba wa akaunti ya Milenia ambapo marekani itaipatia bongo dola kiasi cha 700 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na mapambano dhidi ya ukimwi na malaria na mengineyo.

Rais George Bush wa Marekani na Rais Jakaya Kikwete wakitia saini msaada mkubwa wa $700 Million kutoka serikali ya Marekani, mkataba huo umekusudia kuisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo ujenzi wa barabara tatu ambazo ni barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga,Tunduru Songea hadi Mbambabay na barabara ya Horohoro hadi Tanga na pia msaada wa umeme katika mkoa wa Kigoma. Aidha mara baada ya kutia saini mkataba huo Rais Bush na Rais Kikwete walitembelea hospitali ya Amana iliyopo Ilala, ambayo imepata mafanikio makubwa katika mradi wa mapambano dhidi ya Ukimwi ambao pia umedhaminiwa na serikali ya Marekani.

Rais Bush akifafanua jambo mbele ya viongozi wa serikali na waandishi wa habari leo Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Wakuu wa nchi, akiwemo Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Makamu wa rais Dr. Shein walishuhudia kusainiwa kwa mkataba mkubwa kabisa wa mamilion ya fedha leo asubuhi Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi Condoleeza Rice akiwasalimia wananchi Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Rais Bush na mwenyeji wake Rais Kikwete walitembelea hospitali ya Amana iliyopo Ilala, Dar es Salaam.

Rais Bush na Rais Kikwete wakiwa hospitali ya Amana, Ilala, huku rais Bush akiwasabahi wagonjwa waliohudhuria katika hospitali hiyo na rais Kikwete akimpoza mtoto aliyekuwa akilia na kuumwa.

Hapo hapo, Mama wa kwanza wa Marekani Bi Laura akimkabidhi ufunguo wa gari la wagonjwa katika ofisi za taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) jijini Dar es Salaam.

Mama wa kwanza Salma Kikwete na Mama wa kwanza wa Marekani Mama Laura Bush wakizindua The National Plan of Action, Pamoja Tutaweza, katika ofisi za WAMA jijini Dar es Salaam leo.

Mama wa kwanza wa Tanzania Bi Salma Kikwete akimkabidhi Bi Laura Bush baadhi ya 'brochure' za miradi ya taasisi hiyo.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©