Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Tanzania yatanua matawi ya utalii

22/02/2008

Matangazo ya Tanzania kuanza kuonekana kwenye mabasi ya London na uwanja wa ndege wa Heathrow

Kuanzia wiki ijayo Serikali ya Tanzania itazindua mpango wa kuitangaza Tanzania kwa kuweka matangazo yake kwenye mabasi ya abiria na uwanja maarufu wa ndege wa Heathrow.

Mpango huo utakuwa wa miezi sita. Kwa mujibu wa barua za mwaliko kwenda kwenye vyombo mbalimbali vya habari hapa Uingereza, zilizosambazwa na kampuni ya Jambo Publication inayoratibu matangazo hayo ilisema uzinduzi huo utafanyika katika ubalozi wa Tanzania uliopo Bond Street, katikati ya jiji la London.

Taarifa hiyo ilisema mgeni rasmi katika uzinduzi huo atakuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Maajar, lakini pia Wizara ya Utalii itawakilishwa na Katibu Mkuu, Blandina Nyoni na maofisa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB).

Taarifa ilisema uzinduzi huo utakuwa matangazo manne yatakayokuwa katika sehemu ya kuchukulia mizigo na inatarajiwa kwamba watu milioni 4.6 watayaona wakati kampeni hiyo itakapokamilika.

Sehemu hiyo ipo karibu na idara ya uhamiaji ambayo abiria wanaweza kuyaona matangazo hayo hata wakiwa sehemu ya uhamiaji, jambo ambalo linaweza kuleta mvuto mkubwa kwa watumiaji wa uwanja huo. Mbali na Heathrow, pia katikati ya London kutakuwa na mabasi 100 yatakayokuwa na matangazo hayo na inakadiriwa zaidi ya watu milioni 30 watakuwa wakiyaona kila wiki.

Matangazo hayo yatakuwa yakionyesha mlima Kilimanjaro, Tanga la jahazi, Simba, Swala, Chui na Tembo anuani ya mtandao wa TTB na Wizara ya Utalii, huku yakiwa na maneno "The Land of Kilimanjaro and Zanzibar", "Discover the wonders of the world" na "Have you been there?"

Mwaka ujao wa fedha kuna uwezekano mkubwa kuweka matangazo kwenye treni za chini ya ardhi "underground" na kwenye viwanja vingine vikubwa vya ndege vya Gatwick, Manchester na Birmingham.

Kampuni ya Jambo ndiyo inayochapisha jarida la Jambo Tanzania linalosambazwa katika balozi mbalimbali za Tanzania.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©