![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Muwafaka wa Kenya29/02/2008
Rais Mwai Kibaki (kushoto) na Kiongozi
Mkuu wa chama cha Upinzani nchini Kenya cha HATIMAYE mahasimu wakubwa katika siasa za Kenya, Rais Mwai Kibaki na kiongozi wa Chama cha ODM, Raila Odinga, wamekubaliana kimsingi kuundwa kwa serikali ya mseto nchini humo. Viongozi hao wawili walitia saini makubaliano hayo ambayo yanapewa nafasi kubwa ya kumaliza hali ya uhasama wa kisiasa nchini humo, uliodumu tangu kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais Desemba 30, mwaka jana. Makubaliano hayo ambayo yamezipa ushindi pande zote mbili, ule wa Rais Kibaki na Odinga, yalifikiwa kutokana na jitihada za jumuiya ya kimataifa zilizokuwa zikiongozwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, aliyekuwa akisaidiwa na watu wengine wawili maarufu Afrika, Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Graca Machel, ambaye ni mke wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Aidha, kufikiwa kwa makubaliano hayo jana kulichangiwa pia na juhudi za Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika ( AU), Rais Jakaya Kikwete, ambaye tangu juzi alikuwa nchini Kenya kuyapa mazungumzo hayo msukumo. Uamuzi wa Kikwete kwenda Kenya ulikuja siku ile ile Annan ambaye ndiye msuluhishi mkuu wa mgogoro huo alitangaza kusitisha kwa muda mazungumzo hayo kutokana na pande zinazohusika kusuasua kufikia maamuzi. Aidha, kabla ya Kikwete kwenda Kenya, siku chache zilizopita alikuwa amepokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Kibaki uliowasilishwa Ikulu Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Kenya, Kalonzo Musyoka. Kwa upande mwingine, kufikiwa kwa makubaliano hayo, kumehitimisha machafuko ambayo yamegharimu maisha ya Wakenya wapatao 1,000 huku wengine zaidi ya 300,000 wakihangaika baada ya kupoteza makazi yao. Akizungumza muda mfupi baada ya Kibaki na Odinga kutiliana saini makubaliano hayo, Annan alisema: “Yalikuwa muhimu ili kuinusuru nchi hii.” Kwa mujibu wa makubaliano hayo, serikali ya mseto baina ya vyama hivyo itaundwa kwa kuangalia nguvu ya chama katika bunge la nchi hiyo. Aidha, chini ya makubaliano hayo, chama chenye wabunge wengi ndicho kitakachounda serikali, hatua ambayo kwa namna yoyote ile inampa Raila nafasi kubwa ya kuchukua wadhifa huo mara tu baada ya Bunge kuridhia muafaka huo wa jana. Akitangaza misingi mingine ya makubaliano hayo, Annan alisema waziri mkuu atakayeteuliwa atathibitishwa na bunge na yeye ndiye atakayekuwa mkuu wa shughuli za kila siku za serikali. “Katika makubaliano hayo waziri mkuu mpya atakuwa na mamlaka ya kusimamia shughuli za serikali,” alisema Annan. Mbali ya waziri mkuu, vyama viwili, kile cha PNU na ODM, kila kimoja kitatoa naibu waziri mkuu na hivyo kufanya wadhifa huo kushikwa na watu wawili. Annan alisema mgawanyo wa nyadhifa katika serikali mpya ikiwa ni pamoja na ile ya waziri mkuu na manaibu wake wawili, utatokana na wingi wa wabunge wa kila chama ndani ya bunge. Kutokana na makubaliano hayo, Annan aliwataka Wakenya kuunga mkono makubaliano hayo, akisema: "Kazi ya maridhiano na ujenzi wa taifa sio kwa viongozi pekee. Ni lazima ifanywe na kila upande, kijiji, na taifa zima.
"Ninatoa wito kwa Wakenya kuunga mkono
hatua hii, ili Kenya iweze kurejea katika nafasi yake ya ushawishi wa
kimaadili na injini ya uchumi wa Afrika. Na ningependa kuwahakikishia
kuwa marafiki zenu wa Afrika na jamii ya kimataifa wako nyuma yenu."
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||