![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Matangazo ya utalii wa Tanzania yaanza04/03/2008
Uzinduzi wa matangazo ya kuvutia watalii Tanzania umeanza rasmi mjini London. Pichani juu kutoka kushoto naibu Balozi, Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Maajar, Katibu Mkuu Maliasili na Utalii, Bi Blandina Nyoni, Mkurugenzi wa Jambo Publications Bw. Juma Pinto, wakiwa katika picha ya pamoja nje ya basi la London lenye matangazo ya Tanzania.
Jumla ya mabasi 100 (mia moja) yana matangazo ya Tanzania
Katibu mkuu wizara ya utalii Mh. Blandina Nyoni (kulia) akiongea na balozi wetu hapa UK Mh. Mwanaidi Maajar kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa matangazo kwenye mabasi ya London leo ubalozini London. Hatutangazi Utalii UK kwa matatizo ya Kenya (Na mwandishi maalum, London) SERIKALI ya Tanzania imesema haikufanya kampeni ya matangaza ya utalii nchini Uingereza kwa sababu ya matatizo ya Kenya, bali ni mpango ambao ulikuwepo muda mrefu kabla ya matatizo hayo ya kisiasa yalityotokea nchini huko hali iliyofanya kupungua kwa idadi ya Watalii kwa nchi za Afrika Mashariki wanaotoka Ulaya. Akizungumza katika uzinduzi kampeni kubwa ya matangazo ya Utalii hapa Uingereza juzi katika ubalozi wa Tanzania, Katibu Mkuu Wizara ya Malisili na Utalii,Bi Blandina Nyoni alisema Serikali ilishaweka bajeti yake ya matangazo tangu mwaka uliopita wa fedha na sasa kinachofanyika ni utekelezaji. Bi Nyoni alisema awali Serikali ya Tanzania ilifanya kampeni kama hii kule Marekani mapema mwaka jana na kuzindua matangazo kwenye televisheni ya CNN, hivyo awamu iliyobaki ilikuwa ni Ulaya na kuichagua Uingereza kwani ndiyo inayoongoza kuleta watalii wengi hadi sasa. Katika uzinduzi huo uliohudhuliwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani, wafanyabishara, wawekezaji na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii,ulifuatia kukatwa kwa utepe wa basi moja lililokuwa nje ya ubalizi wa Tanzania kuashilia kuzinduliwa rasmi kwa kampeni hiyo. Alisema hivi sasa Tanzania imeamua kujitangaza na kuvitangaza vivutio vyake katika kuhakikisha tunapata watalii wengi zaidi ili tuweze kuongeza pato la Taifa na haifanyi hivyo kwa matatizo ya Kenya, hali ambayo imeathili kwa kiasi fulani kupungua kwa watalii, lakini sasa hali imerudi kawaida. “Kweli tunaishukuru sana kampuni ya Jambo Publication kwa kutufanyia kazi hii, kweli imefanyika kama sisi tulivyotaka na tuna imani hata huko siku za baadae tutaendelea kufanya nao kazi, kwani wana uchungu na nchi yao na pia wanaijua vilivyo,” alisema Bi Blandina. Alisema Serikali inakusudia kuongeza matangazo zaidi ya utalii kwa Uingereza kwa sababu imekuwa ikichangia sehemu kubwa ya pato la Taifa kutokana na watalii wengi wanaongia nchini, hali inayofanya idadi yao kuongezeka mwaka hadi mwaka. Bi Nyoni alikitoa tathmini ya watalii wa Uingereza wanaotembelea Tanzania alisema mwaka 1997 walifika watalii 25,000 hadi 2006 walifika 69,160 na mwaka 2007 idadi hiyo iliongezeka. Tanzania imeweka matangazo 100 kwenye mabasi ya London na matangazo manne katika uwanja wa ndege wa Heathrow.Matangazo hayo yameratibiwa na kampuni ya Kitanzania ya Jambo Publication chini ya Mkurugenzi wake, Bw. Juma Pinto. “Tutashilikiana na balozi zetu kuhakikisha tunafanya juhudi kubwa za kuhakikisha tunafanikiwa katika kuutangaza utalii na kuna mikakati mingi tumeifanya na sasa ni utekelezaji wake unaendelea,” alisema Blandina Nyoni. Alisema wameamua kuanzia matangazo yao kwa nchi za Ulaya hapa Uingereza kwa sababu ndiyo sehemu muhimu hapa Ulaya, kwani ndiyo nchi ambayo inapokea wageni wengi kuliko nchi nyingine yoyote hapa Ulaya, hivyo kujitangaza hapa ni sawa na kujitangaza duniani. Awali Balozi wa Tanzania Uingereza, Mwanaidi Senare Maajar alisema tayari ubalizo wake umekuwa ukifanya kazi kwa karibu na wizara ya utalii tangu mwaka jana na hivi sasa wao mbioni kutafuta wafanyakazi watakaofanya kazi katika sekta ya utalii hapa ubalozini. Balozi Maajar alisema Uingereza ni ufunguo muhimu katika sekta ya utalii wa Tanzania, hivyo wameweka mikakati mikubwa ya kufanyia kazi soko la utalii ili kuongeza idadi ya watalii na pia lengo la pili ni kuitangaza Tanzania. “Tanzania tuna vivutio vingi sana ambavyo vinahitajika kutangazwa,na haya yaliyotangazwa katika matangazo ya sasa ni vichache tu katia ya vivutio vingi,serikali yetu inafuata misingi ya demokrasia na hata hali ya kisiasa ni nzuri na wananchi wake wana upendo mkubwa sana,” alisema Balozi Maajar.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||