Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Ajali ya magari njia ya Dubai na Abu Dhabi

11/03/2008

Ajali ya magari zaidi ya mia ambayo yamelundikana na mengine kuungua moto katika ajali iliyotokea katikati ya njia ya Dubai na Abu Dhabi iliyotokea Jumanne ya tarehe 11/03/2008.

Ajali hiyo ambayo imesababishwa na ukungu uliotanda kwenye njia ambao umepunguza uwazi wa kuona mbali chini ya mita 50 ambayo ni sawasawa na nusu kiwanja cha mpira wa miguu.

Ajali hiyo imesababisha magari zaidi ya mia kugongana yakiwemo mabasi yanayochukua wafanyakazi kutoka Abu Dhabi kuelekea bandari ya Jebel Ali ambayo ipo Dubai.

Juu ni ramani inayoonyesha sehemu ambayo iliyotokea ajali hiyo.

Polisi ya UAE imetangaza magari 25 yameshika motomoto baada ya ajali kutokea.

Majeruhi waliwahiwa kwenye hospitali za karibu ambazo zipo na ajali, hospitali mojawapo ikiwemo Mafraq Hospital ambayo ipo Abu Dhabi.

Baadhi ya majeruhi waliowahishwa hospitali.

Walioshuhudia walisema ajali ilikuwa ni 'disaster'; na mlolongo wa magari yalisimama kutembea kwenda njia zote mbili (Abu Dhabi na Dubai).

Wanazimamoto wakiondoa vifusi vilivyosambaratika kutokana na ajali hiyo.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©