Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Michael Jackson na familia yake kuhamia UK

13/03/2008

Muimbaji mashuhuri duniani Michael Jackson ameamua kuuza nyumba yake (ranchi) ambayo aliita 'Neverland' ipo katika mabonde ya California. Mji ambao upo 'Neverland' ni mji mdogo sana ambao upo California wenye idadi ya wakazi wapatao 1000 (elfu moja) na wenye uwezo wa juu.

'Neverland' ina eka 2500 (elfu mbili mia tano). Mwezi uliopita, Michael Jackson alitangaza kuuza nyumba yake hiyo na baada ya mjadala mrefu (ambao ulichukua masaa 11) na mwanasheria wake ambao ulifanyika Alhamisi ya tarehe 13/03/2008. Mwishowe, wamefikia uamuzi ya kuwa ataiuza nyumba yake kwenye mnada ambao unatarajiwa kuwa tarehe 19/03/2008, Jumatano ijayo, na ana mpango wa kuhamia Devon, UK.

Kaka yake Michael Jackson, Tito Jackson, alitembelea Devon sehemu za Barnstaple (kusini-magharibi mwa UK) kuangalia nyumba ambayo itamfaa Michael Jackson na familia yake kuhamia. Tito alisema wanafikiria kununua nyumba mbili ikiwamo ya Michael Jackson ili wawe na sehemu ya kupumzikia wakati watakapohitaji katika hiyo nyumba nyingine. Tito kaielezea Devon, 'North Devonshire coast' ni sehemu kimya na iliyotulia.


View Larger Map

Tito ameshatoa 'offer' ya nyumba mbili katika mji wa Barnstaple ambao una wakazi 34000 (elfu thelathini na nne), na sehemu ya nyumba hizo zimehifadhiwa.

Mlinzi wa familia ya Jackson, na vilevile rafiki yake Michael Jackson (Matt Fiddes) ameeleza kuwa ni kweli jambo hilo lipo njiani na litakuwa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©