Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Queen azindua rasmi kituo cha (Heathrow Terminal 5)

14/03/2008

Queen Elizabeth II amefungua rasmi kituo kipya cha 'Terminal 5' cha uwanja wa ndege wa London Heathrow. Baada ya miaka 15 ya upangaji na upanguaji na upinzani wa kituo hicho, leo imefikia kikomo na sherehe rasmi za kufungua kituo cha tano cha uwanja wa ndege wa Heathrow na Malkia Elizabeth.

Sherehe hizo zimefanyika ndani ya masaa 24 baada ya mtu asiyejulikana kuvunja sheria ya usalama na kuparamia waya za kiwanja ndege hicho na kuingia ndani.

Maafisa wa usalama waliwahi kumkamata mtu huyo karibia na njia ya kupitia ndege.

Ulinzi mkubwa uliwekwa wakati Malkia alipotembelea kituo hicho kipya huku akikaribishwa na mamia ya wafanyakazi na wajenzi wa kituo hicho.

Hapo hapo Malkia alitambulishwa na mashujaa rubani wa ndege ya (BA) Boeing 777 ambao waliishusha ndege hiyo kwa usalama katika ajali iliyotokea Januari mwaka huu.

Malkia alielezea kituo hicho kipya kama ni kituo kinachopambana na maendeleo ya karne mpya duniani kote. Kituo hicho (Terminal 5) kitakuwa kinatumika kwa ndege za British Airways tu, alivyoelezea mkuu wa BA bwana Willie Walsh

Kiwanja hicho kina ukubwa wa viwanja 50 vya mpira wa miguu, sehemu ya kupumzikia wasafiri (lounge) ambayo inasemekana ni kubwa kuliko (lounge) zote duniani, ina maili 11 ya kupokelea na kusafirishia na kuhifadhia mabegi, ina maduka ya kifahari na sehemu za vyakula ambazo zimependekezwa na Gordon Ramsay wa programu ya TV (Kitchen Nightmares).

Vilevile kutakuwa na vyumba maalum vya abiria wakitaka kupumzika wakiwa wakila vyakula vyao huku wakisubiri usafiri wao.

Kituo hicho kitaanza rasmi kutumiwa na abiria tarehe 27/03/2008, lakini inasemekana kuwa kutokana na wingi wa ndege za BA na abiria wake, itabidi abiria wengine waendelee kutumia vituo vingine kama (Terminal 3, 4, n.k).

BAA (British Airpots Authority) wamesema kuwa lazima kuwe na mpango mzuri wa abiria wanaosafiri kwenda nchi za nje na wale wanaosafiri humu-humu nchini, kwasababu wote wanatumia (lounge) moja.

Wasimamiaji wa kituo hicho (BAA) wamesema siku za mbele abiria wote watakaosafiri katika kituo hicho itabidi wachukuliwe alama za vidole vyao (fingerprints) watakaposafiri. Wamesema kufanya hivyo itasaidia kuleta hali ya usalama na vilevile itapunguza wizi wa kimachomacho (fraud). Mfano, kwasababu (lounge) ya kusafiria ni moja kwa wasafiri wa kitaifa na wasafiri wa humu nchini, abiria wa kitaifa anaweza kubadilishana tiketi na abiria wa humu nchini kirahisi na kusafiria tiketi hiyo bila ya kupitia kitengo cha uhamiaji (immigration control).

Kwahivyo kila anayetaka kuingia ndani ya ndege atachukuliwa alama za vidole vyake kabla ya kuingia mlangoni hapo hapo. Lakini BAA wamesema rekodi hizo za alama ya vidole zitaharibiwa siku hiyo hiyo na hazitohifadhiwa.

Ujenzi mkubwa unaongezeka wa usafiri wa 'underground' ili uweze kuhudumia abiria watakaosafiria uwanja huo.

Bonyeza picha hapo juu uangalie mambo yanayogusia kituo hicho kipya.

Kwa ufupi:

- Gharama: 4.5 billion

- Ujenzi umeanza Septemba 2002

- Milango ya kusimamia ndege: 60 (ifikapo mwaka 2010)

- Paki za magari: 3,800

- Vituo vya kujihudumia tiketi (self service check-in): 96

- Vituo vya tiketi vya kawaida (check-in): 54

- Mistari ya kupita ya Usalama: 20

- Mabegi yanahudumiwa kwa muda wa saa moja ni: 12,000

- Lifti za abiria kwenda safu zingine: 192

- Mikanda ya umeme ya kusafirishia abiria: 105

- Maduka ya vitu mbalimbali: 112

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©