![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Mwenge wa Olimpik kuwasili London mwezi Aprili23/03/2008
BARA la Newham, East London litaupokea mwenge wa Olimpik Jumapili ya tarehe 06/04/2008 katika mitaa ya Stratford kuashiria uwenyeji wa Olimpik ya mwaka 2012 baada ya Olimpik ya Beijing, China ambayo itakuwa mwaka huu 2008. Mwenge huo utawashwa Ugiriki (Greece) katika mji wa Olimpia ambapo ndipo kulipoanzia michezo ya Olimpik. Mara utakapowashwa mwenge huo siku ya Jumatatu ya tarehe 24/03/2008, utazungushwa katika miji 22 duniani ambayo ipo katika mabara yote matano, ukiwamo mji wa London. Mwenge huo utakapofika London tarehe 06/04/2008, utawashwa na utaanzia Meridian Square, Stratford (bonyeza hapa kwa ramani) mnamo saa 10 jioni halafu utaelekea Greenwich Dome (iliyokuwa ikiitwa Millenium Dome) kwa kumalizia sherehe hizo na vimbwanga mbalimbali. Kutakuwa na tafrija mbalimbali za kifamilia na mengineyo kama fataki, carnival (za barabarani) na watumbuizaji tofauti wakitumbuiza katika barabara za East London na kutakuwa na baadhi ya michezo itakayochezwa katika Olimpik, vilevile kwa watakaohudhuria kutakuwa na fursa ya kuendesha baiskeli, mitumbwi, na makasia ambayo yatakuwepo siku hiyo. Vilevile kutakuwa na viburudisho vya muziki tofauti, chai, kahawa, n.k. Kufika huko, tumia usafiri ufuatao: DLR Underground: Jubilee Line na Central Line Mabasi: 25, 69, 86, 104, 108, 158, 238, 241, 257, 262, 276, 308, 473, D8, S2
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||