Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Jeshi la Tanzania na Umoja wa Afrika laingia Komoro

25/03/2008

Majeshi ya umoja wa Afrika yakiongozwa na majeshi yetu ya Tanzania pichani juu, wameutwaa mji mkuu wa Anjouan nchini Komoro katika kumng'oa rais aliyejipachika urais nchini humo Kanali Mohammed Bacar. Kanali Bacar alijipachika urais kinguvu bila ya ridhaa ya serikali ya Komoro kwa kutumia nguvu ya ugaidi. Jeshi la AU likiongozwa na jeshi la Tanzania, limeingia nchini humo kumng'oa rais huyo, kuleta usalama na kuipa serikali ya Komoro nchi yao kuiongoza kisalama.

Majeshi ya Tanzania wameutwaa mji wa Anjouan kiulaini kabisa bila hata ya mwanajeshi mmoja kufa au kujeruhiwa. Majeshi hayo kabla hawajaingia katika miji mikubwa waliuchukua uwanja wa ndege kwanza halafu wakasambaratika katika vitongoji vingine katika visiwa vya Komoro ukiwemo mji wa Mutsamudu.

Asubuhi ya leo, risasi na makombora yalisikika wakati jeshi la Tanzania lilipoingia katika miji ya Komoro kwa njia ya maji.

Wanajeshi wa Tanzania wakiongoza majeshi ya umoja wa Afrika walishangiliwa kwa shangwe na vifijo katika mitaa ya visiwa vya Komoro baada ya majeshi hayo kuchukua nchi.

Kabla ya jeshi kuingia katika visiwa hivyo, wananchi wote walitupiwa vikaratasi (leaflets) vya kuwajulisha nini kinachoendelea na nini kitakachoendelea.

Kuingia katika nchi hiyo imefuata baada ya mwaka mmoja wa Kanali Mohammed Bacar ambaye ni kiongozi wa jeshi la ugaidi kuchukua uraisi kinguvu na kuendesha nchi kijeshi bila ya kuleta maendeleo yoyote katika nchi hiyo. Mpaka sasa Kanali Mohammed Bacar hajulikani halipo.

Mungu ibariki Tanzania!

Mungu ibariki Afrika!

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©