![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Bi Salma Kikwete kusisitiza kutokomezwa kwa mila zinazombagua mtoto wa kike27/03/2008
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoa wito kwa jamii ya Kitanzania kupiga vita mila na desturi zinazombagua mtoto wa kike na badala yake kumpa elimu bora na malezi bora ili kumwezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za ujenzi wa taifa. Mama Kikwete aliyasema hayo alipokuwa anafungua mkutano wa kushirikishana uzoefu wa masuala yanayohusu kupunguza unyanyasaji kijinsia dhidi ya wanawake uliofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeandaliwa na Chama Cha Wanawake na Ukimwi Afrika Tawi la Tanzania (Society for Women and AIDS in Africa - Tanzania Branch SWAA-T). “Taasisi zetu katika kutoa michango ya utekelezaji wa sera ya serikali, ziwe na mipango madhubuti na shughuli zitakazomwezesha mwanamke wa kitanzania kujiamini, kujitegemea na kuwa na familia bora yenye afya njema,” alisema. Mama Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) amesema taasisi yake imeamua kwa dhati kupambana na changamoto zitokanazo na mila na desturi mbaya kwa kutoa kipaumbele kwenye elimu ya mtoto wa kike na uwezeshwaji wa wanawake kiuchumi kama njia ya kukomesha unyanyasaji wa wanawake. Mke wa Rais alisema pia kuwa hali duni za maisha zimesababisha watoto kuhusishwa katika biashara ya kutemebeza vyakula mitaani hususan nyakati za usiku jambo ambalo alisema huwaweka katika mazingira hatarishi. “Hivyo basi katika kipindi hiki ambacho maadili yamemonyoka ni wazi kuwa tunapofanya hivi tunawaweka watoto katika hatari ya kutendewa vitendo vya unyanyasaji au ukatili wa kijinsia,” alisisitiza. Aliendelea kusema kuwa suala la unyanyasaji wa kijinsia linaanzia katika malezi wanayolelewa watoto mbayo huleta athari kisaikolojia na kimtazamo akifafanua kuwa katika familia nyingi nchini mtoto wa kike hufanyishwa kazi nyingi kiasi cha kukosa muda wa kujisomea huku yule wa kiume akiachwa kucheza. “Inasikitisha kuona kwamba mpaka kufikia karne hii, bado ziko familia zinadhani kwamba elimu kwa mtoto wa kike si muhimu na inapotokea nafasi ya kusoma mtoto wa kiume anapewa kipaumbele,” alisema. Mama Kikwete alisema kuwa itakuwa ni ndoto kwa jamii ya Kitanzania kufikia maendeleo iwapo unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia utaachwa kuendelea na kwamba unyanyasaji wa kijinsia ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Akisoma risala kwa niaba ya wanachama wa SWAA-T, mratibu wa mkutano huo Dr. Naomi Mpemba alisema kuwa malengo makuu ya chama hicho ni kuwawezesha wanawake na watoto kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotokana na maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kutoa elimu kwa wanawake na vijana, kuhudumia wagonjwa wa ukimwi majumbani na kutoa elimu ya lishe bora kwa wajawazito. Dr, Naomi alisema kuwa kati ya mwaka 2005 hadi sasa jumla ya watoto 11,250 wamenufaika na malezi yaliyoratibiwa na chama hicho kupitia kwa wazazi na walezi waliopatiwa mafunzo kupitia chama hicho.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||