Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Vijana wa Zenjydar Team wameanza mazoezi

30/03/2008

Vijana wa jamii ya Waswahili wa East London wameanza mazoezi katika programu ya 'Come n' Join' programme, ni programu ambayo imeandaliwa na Zenjydar Community Association ya kuwafanya vijana wawe katika hali ya kiafya na kuendeleza ustadi wao wa mpira wa miguu. Pili (shoto) kocha Steve na pili (kulia) Katibu wa Zenjydar Bw. Farid.

Pichani (kushoto) ni Mwenyekiti wa Zenjydar Community Association Bw. Saleh Jaber na Kocha mpya wa Zenjydar Team Bw. Steve wakibadilishana mawazo katika uangaliaji wa mahudhurio na nidhamu ya watoto uwanjani na vipi kocha huyo ataweza kuangalia maendeleo ya ustadi wa kila mtoto watakapokuwa uwanjani.

Leo (30/03/2008) ilikuwa ni siku ya kwanza ya mazoezi ambayo ilitangazwa kwa njia ya mdomo tu. Mwenyekiti wa Zenjydar Community Association Bw. Saleh Jaber amesema kuwa matangazo rasmi ya programu hiyo yapo njiani na yatatangazwa katika njia zote za kuwafikia jamii na leo ilikuwa kama 'soft opening'.

Kabla vijana hao hawajaanza mazoezi leo, Mwenyekiti aliwatambulisha vijana wote waliohudhuria na kocha wao Bw. Steve ambaye wamekutana nae kwa mara ya kwanza hapo uwanjani.

Bw. Steve (CRB cleared) ambaye ni mtu wa kutoka Uganda, au kwa jina lingine anapendelea kuitwa Farouq (ni jina ambalo kalipata baada ya kusilimu hivi karibuni) amesema yeye ni mtu ambaye anapenda kazi ya ukocha na anapenda kufundisha vijana ili apate kuendeleza ustadi wake zaidi ambao utamsaidia katika kazi zake za baadaye kwenye fani ya mpira wa miguu na vilevile angependa kuona maendeleo ya ustadi wa vijana kwenye mpira wa miguu. Zenjydar imempokea na imeahidi kumpatia mafunzo zaidi 'professional' ya ukocha.

Mwenyekiti wa Zenjydar katika hotuba ya dakika 5 aliyoitoa kwa vijana waliohudhuria leo alisema, kwanza kabisa kafurahi kuwa vijana na watoto waliohudhuria wameitika mwito wa kuja kushirikiana na wenzao katika fani ya kucheza mpira wa miguu katika jamii yao na kupata kujuana na vijana wenzao katika jamii yao.

Vilevile amewaeleza kuwa anawashukuru wazee wa vijana hao kuwapa fursa watoto wao kuja kujiendeleza ustadi wao na kujiweka wao wenyewe kwenye hali ya kiafya na kasisitiza wazee kujikurubisha sana kuwa 'support' watoto wao katika programu kama hizi na kuwa pamoja katika jamii ili kuleta maendeleo ya watoto (kimwili na kiakili) na vilevile kushirikiana na viongozi wa programu ambao vilevile wanaangalia tabia za watoto wakiwa mazoezini na kuwafanya wawe watoto wenye 'discipline' wanapokuwa uwanjani na baada ya kuwa uwanjani.

Mazoezi yatakuwa kila wikiendi Jumamosi 9:30am mpaka 12:00pm; na Jumapili 2:30pm mpaka 6:00pm, West Ham Park. Kwa kupata habari zaidi za programu ya (Come n' Join) bonyeza hapa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©