Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Kamati ya Zenjydar yakutana na Mhe. balozi Mwanaidi Maajar

31/03/2008

Kamati ya Zenjydar Community Association imekutana na Mhe. balozi wa Tanzania nchini United Kingdom, Mhe. Mwanaidi Sinare Maajar leo hii ubalozini mjini London. Pichani kutoka kulia Bw. Farid Ahmed Said (katibu wa Zenjydar), Bw. Saleh Jaber (mwenyekiti wa Zenjydar), Mhe. balozi Mwanaidi Maajar, Bw. Mrisho Senga (muweka hazina Zenjydar), Bi. Sofia Issa (elimu ya jamii kwa watoto na wanawake Zenjydar) na Mhe. Athman Mashanga (mkuu wa elimu na utamaduni Tanzania High Commission).

Mwenyekiti wa Zenjydar Community Association Bw. Saleh Jaber, aliona ni muhimu kwa kamati yake kuzitambulisha huduma zinazotolewa na Zenjydar Community Association hapa nchini United Kingdom na kutambulisha mtazamo wa baadaye wa Zenjydar Community Association ambayo ni moja ya jumuia ndogo ndogo ambazo zipo ughaibuni katika kusaidia mapengo madogo madogo ya kuleta maendeleo nyumbani Tanzania.

Mheshimiwa balozi Mwanaidi alisisitiza kuwa ni muhimu jumuia ndogo ndogo ambazo zipo ughaibuni (United Kingdom) kujishirikisha na kujenga nchi yao. Alisema kuwa yupo tayari kusikiliza jumuia yoyote ambayo itamkurubia kwa kutaka misaada midogo midogo ya kuleta maendeleo nyumbani.

Tarehe 17/04/2008, Alhamisi, Rais wa Tanzania, Mhe. Kikwete atakuja UK katika ziara yake ya mkutano wa 'Diaspora' ambao ni mkutano unaogusia kuwapa nafasi Watanzania, jumuia ndogo ndogo na jumuia zingine ambazo zipo hapa UK zenye mtazamo wa kusaidia nyumbani Tanzania.

Kujihusisha katika mkutano huo bonyeza hapa chini halafu nenda kwenye 'Registration'.

http://africarecruit.com/Tanzania_Event/index.php

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©