Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Mwenge wa Olimpik unakuja London na Dar es Salaam, Tanzania

04/04/2008

BARA la Newham, East London litaupokea mwenge wa Olimpik Jumapili ya tarehe 06/04/2008 katika mitaa ya Stratford kuashiria uwenyeji wa Olimpik ya mwaka 2012 baada ya Olimpik ya Beijing, China ambayo itakuwa mwaka huu 2008.

Mwenge huo umeanzia kwa kuwashwa moto wake nchini Ugiriki (Greece) tarehe 24/03/2008 katika mji wa Olimpia ambao ndio mji ulioanzishiwa michezo ya Olimpik na utawaka kwa siku 130. Mwenge huo utazungushwa katika miji 22 duniani ambayo ipo katika mabara yote matano, ikiwamo mji wa London, U.k, na Dar es Salaam, Tanzania.

Inasemekana kihistoria ndio mara ya kwanza mwenge huo kutembea kwa urefu wa kilomita 137,000 kwa kupitia miji muhimu duniani kote.

Mwenge huo utafika London tarehe 06/04/2008 baada ya kutoka Wembley Park, utawashwa na utaanzia Meridian Square, Stratford, Newham (bonyeza hapa kwa ramani) mnamo saa 10 jioni halafu utaelekea mchaka-mchaka mpaka Greenwich Dome (iliyokuwa ikiitwa Millenium Dome) kwa kumalizia sherehe hizo na vimbwanga mbalimbali.

Kutakuwa na tafrija mbalimbali za kifamilia na mengineyo kama fataki, carnival (za barabarani) na watumbuizaji tofauti wakitumbuiza katika barabara za East London na kutakuwa na baadhi ya michezo itakayochezwa katika Olimpik, vilevile kwa watakaohudhuria kutakuwa na fursa ya kuendesha baiskeli, mitumbwi, na makasia ambayo yatakuwepo siku hiyo. Vilevile kutakuwa na viburudisho vya muziki tofauti, chai, kahawa, n.k.

Rais Jakaya Kikwete leo (Ijumaa, Aprili 4, 2008) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Bwana Liu Xinsheng. Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu mjini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Mhe Rais na Balozi Xinsheng wamezungumzia uhusiano wa muda mrefu na wa kindugu kati ya nchi hizo mbili.

Balozi Xinsheng pia ametumia mazungumzo hayo kumwelezea Mhe. Rais kuhusu Mwenge wa Olimpiki ambao utakimbizwa nchini Tanzania, Aprili 13 mwaka huu.

Tanzania ni moja ya nchi 22 duniani, na nchi pekee katika Bara la Afrika, ambako mwenge huo utakimbizwa katika mzunguko wake wa dunia kabla ya kurejea Beijing, China tayari kwa Michezo ya Olimpiki inayofanyika nchini humo baadaye mwaka huu.

Mhe. Rais amefurahishwa na uamuzi wa China kuiteua Tanzania kuwa moja ya nchi ambako Mwenge huo utakimbizwa na kusema kuwa hiyo ni heshima kubwa kwa Tanzania.

Baada ya mwenge huo kupita miji maalum duniani, utapita katika barani China mchaka-mchaka kuelekea katika KILELE cha mlima mrefu duniani (Mount Everest) ambao upo nchini Nepal.

Mwishowe, mwenge utakimbizwa mpaka mjini Beijing kwa mara ya mwisho ya kuanza maonyesho ya Olimpik mnamo tarehe 08/08/2008.

Mwenge wa Olimpik una urefu wa Sentimita 72, Uzito wa gramu 985, Umetengenezwa na madini ya Aluminiamu na moto wake unahimili nguvu ya upepo unaokwenda mpaka spidi ya kilomita 65 kwa saa.

Kufika huko, tumia usafiri ufuatao:

DLR

Underground: Jubilee Line na Central Line

Mabasi: 25, 69, 86, 104, 108, 158, 238, 241, 257, 262, 276, 308, 473, D8, S2

Ramani ya mwenge London: bonyeza hapa

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©