Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Masahihisho ya Uteuzi wa Mhe. Issa Michuzi na Wilaya yake ya Tegeta

05/04/2008

KUNRADHI:

Yote yaliyochapishwa hapo chini tarehe 01/04/2008, siku ya Jumanne, yalikusudiwa kama utani wa April fool's day na SI ya kweli. Yalibainishwa na mwenyewe Kaka Issa Michuzi kwa njia ya barua pepe kwa kusema "...ukweli ni kwamba niliweka kama utani wa April fool's day na haina ukweli wowote. Hivyo si vibaya kwenye posti katika tovuti yenu mkabainisha hivyo ili kuondoa usumbufu kwa wadau sehemu mbalimbali duniani. Ahsanteni sana. Kazi njema."

MJUMBE HAUWAWI! Lakini kila kitu kinawezekana! Ahsante kaka Michu, mwakani tutakuwa makinifu, Hehehe! (Mhariri, Zenjydar)

Habari yenyewe iliyochapishwa tarehe 01/04/2008 ni kama ifuatavyo:

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE LEO AMEMTEUA NDUGU MUHIDIN ISSA MICHUZI KUWA MKUU MPYA WA WILAYA MPYA YA TEGETA ILIYOPO WILAYA YA ILALA, DAR ES SALAAM.

TAARIFA TOKA IKULU IMESEMA UTEUZI HUO, AMBAO UNAANZA MARA MOJA, UNAKUJA SIKU MOJA TU BAADA YA SERIKALI KURIDHIA OMBI LA WAKAZI WA TEGETA KUIFANYA SEHEMU HIYO KUBWA KUWA WILAYA KAMILI, NA KUFANYA DAR ES SALAAM KUWA NA WILAYA NNE - ZIKIWEMO ILALA, TEMEKE NA KINONDONI.

KABLA YA UTEUZI HUO, NDUGU MICHUZI ALIKUWA NI MPIGA PICHA MWANDAMIZI WA MAGAZETI YA SERIKALI YA DAILY NEWS NA HABARI LEO, KAZI AMBAYO IMEBIDI AIAGE ILI KUSHIKA WADHIFA WAKE HUO MPYA.

"HAKIKA NIMEHEMEWA KWANI KAZI YA UKUU WA WILAYA SI NDOGO UKIZINGATIA KWAMBA NDIYO SHINA LA SERIKALI KUU" NDUGU MICHUZI ALISEMA BAADA YA KUHOJIWA NA GAZETI HILI LEO JIONI.

HII SI MARA YA KWANZA KWA RAIS KIKWETE KUTEUA WANAHABARI KUSHIKA NYADHIFA KAMA HIYO, WENGINE WAKIWA NI MH. BETTY MKWASA AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA KOROGWE, NA MH, HALIMA KIHEMBA, MKUU WA WILAYA YA KILOSA. WOTE HAWA NI WANAHABARI.

AKIONGELEA HATMA YA BLOGU YAKE, MH. MICHUZI AMESEMA KWA LUGHA YAKE ANAYOPENDA KUITUMIA KWAMBA ATAENDELEZA LIBENEKE KAMA KAWAIDA HATA KAMA ANGECHAGULIWA KUWA RAIS.

"HII BLOGU NI YA JAMII HIVYO SINTOELEWEKA ENDAPO KAMA NITAAMUA KUIACHA ATI KWA SABABU YA KUPATA WADHIFA SERIKALINI. SIONI NI JINSI GANI NITASHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YANGU KAMA MKUU WA WILAYA MPYA YA TEGETA NA WAKATI HUO HUO KUHUDUMIA JAMII KUPITIA BLOGU YAO HII," ALISEMA MH. MICHUZI.

UAMUZI WA KUIFANYA TEGETA KUWA WILAYA KAMILI UMEFIKIWA BAADA YA KUONEKANA KWAMBA ENEO HILO LILILOPO KASKAZINI MWA JIJI LA DAR ES SALAAM LIMEKUA KWA KASI NA KUWA NA WAKAZI WENGI KIASI YA KWAMBA KUENDELEA KUWA CHINI YA WILAYA INGINE KUNGELETA MATATIZO KWA WAKAZI WAKE.

MHE. MICHUZI ANATARAJIWA KUAPISHWA LEO ASUBUHI NA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM, MH ABBAS KANDORO, KATIKA SHEREHE ZILIZOPANGWA KUFANYIKA KWENYE OFISI ZA MKUU HUYO WA MKOA, ILALA BOMANI.

Samahanini kwa usumbufu mdogo!

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©