Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Ujumbe wa Leo kutoka Dar, "Ya Mungu Mengi"

08/04/2008

Pichani juu ni ujumbe wa leo kutoka Dar es Salaam.

Bi Bahati Iddi Nzimano

Je, wamkumbuka Bi. Bahati Iddi Nzimano? yule dada wa Tabora aliyezaliwa bila mikono na ambaye amekataa kuwa ombaomba mitaani kutokana na ulemevu wake? basi bahati bado anadunda na pamoja na shida ndogo ndogo za kawaida kwa binadamu yeyote anaendelea na maisha kama kawaida.

Hivi sasa yeye ni mjumbe wa taifa wa mkoa wa Tabora katika mkutano mkuu wa chama cha wenye ulemavu nchini na mwaka juzi kwenye uchaguzi mkuu nusura aukwae ubunge kupitia viti maalumu vya wenye ulemavu, lakini bahati haikuwa yake aliambulia kuwa mtu wa tatu.

Bi Bahati alitembelea Dar es Salaam hivi karibuni katika ziara yake ya kikazi na Kaka Michuzi alipata bahati ya kutembelewa ofisini kwake na Bi Bahati ambako hakusita kumuonesha namna anavyoweza kumudu maisha kwa kutumia miguu (kwa kupiga simu ya mkononi kwa kutumia miguu) na mengineyo.

 

 

 

Bado tu hujaamini...

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©