![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
China yajitayarisha kukabiliana na Olimpik ya 200812/04/2008
China inaandaa kikosi maalum cha kukabiliana na Olimpik itakayofanyika mjini Beijing mwaka huu 2008.
Kutokana na wakuu wa ulinzi wa Uchina, kikosi hicho kimeandaliwa kukabiliana na ujinai, ugaidi, uvurumi na mengine yanayohatarisha usalama wa raia na watakaohudhuria Olimpik kwa ujumla.
Polisi wa kikosi maalum wakihusishwa katika mazoezi mbalimbali ya kila siku kuwa tayari na pirika zozote zitakazotokea.
Hapo juu pichani siyo filamu ya kiini macho, hapo ni mikono kavu-kavu
Polisi hao wanafanya mazoezi nchi kavu na ufukoni mwa bahari iwapo kutatokea chochote cha hatari kwa njia ya bahari ambacho si cha kutegemewa.
Pichani, mmoja wa polisi akionekana akimpa maelekezo Ng'ang'a wake jinsi ya kukabiliana na ugaidi. Inasemekana timu hii itachukuwa nafasi kubwa kwenye maeneo yanayozunguka matukio la Olimpik hasa viwanja vya mpira wa miguu.
Beijing hivi sasa, ulinzi umekuwa jambo aula baada ya mambo yaliyojitokeza hivi karibuni kuhusu Tibet.
Kikosi maalum kikifanya mazoezi kwenye theluji (snow) kwa kupakaza barafu kwenye mwili kuonyesha ukakamavu wa mwili.
Kikosi hicho kinaonyesha mbinu za kukabiliana nchi kavu na ndani ya maji.
KUNG FU imezaliwa China
Kikosi cha ulinzi kikifanya mazoezi ya kukabiliana na washabiki wa mpira wa miguu na yoyote yule mwenye kuleta fujo.
Kikosi hicho kimetengewa sehemu maalum katika ziwa la Wuhan, China, kwa mazoezi ya kukabiliana lolote litakalotokea kwa njia ya maji.
Inasemekana, katika kikosi hichi, watu 600 ziada wameandikishwa iwapo kutatokea na mafuriko bila ya kutarajiwa.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||