Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Je, nani unamtaka awe Meya wa jiji la London?

24/04/2008

Nani atakaye kaa katika jumba la 'City Hall' mjini London baada ya uchaguzi wa Mei mosi?

Tarehe 01/05/2008, wakazi wa London watapiga kura ya kumchagua meya wao mpya wa msimu unaokuja wa jiji la London.

Wafuatao ni waliojitokeza katika kugombea umeya wa jiji la London na mapendekezo ya kufanya iwapo watachaguliwa kuwa Meya wa London.

Jina:

Alan Craig (mgombea uchaguzi kutoka: Christian Choice).

Mapendekezo yake:

1. Atasisitiza watu kuoana badala ya kukaa mbalimbali.

2. Atasimamisha mapendekezo ya kujengwa msikiti mkubwa wa West Ham.

Jina:

Lindsey German (mgombea uchaguzi kutoka: Left List).

Mapendekezo yake:

1. Kujengwa kwa nyumba za dharura kwa wananchi za halmashauri ya jiji.

2. Kukata bei za usafiri.

Jina:

Winston McKenzie (mgombea uchaguzi kutoka: Independent).

Mapendekezo yake:

1. Kupunguza 'Congestion charges' za katikati ya jiji la London ambazo hivi sasa ni £8.00

2. Kuongeza pesa za kunufaisha miradi ya watoto na vijana.

Jina:

Richard Barnbrook (mgombea uchaguzi kutoka: British National Party (BNP).

Mapendekezo yake:

1. Kuwapa nyumba raia wa 'British' kwanza, kabla ya watu wa kutoka nchi nyingine.

2. Kuwapa wazee walio na pensheni tikiti za usafiri.

Jina:

Matt O'connor (mgombea uchaguzi kutoka: English Democrats).

Mapendekezo yake:

1. Kupigana na jinai na silaha za mkononi mitaani.

2. Kuwapa moyo familia kuwa pamoja na maisha mazuri.

Jina:

Gerard Batten (mgombea uchaguzi kutoka: United Kingdom Independent Party (UKIP).

Mapendekezo yake:

1. Kutokomeza 'Congestion Charges'.

2. Kudhibiti gharama za Olimpik ya London 2012.

Jina:

Sian Berry (mgombea uchaguzi kutoka: Green Party).

Mapendekezo yake:

1. Atahakikisha magari yote yapitayo njia za ndani za wakazi wa London yanakwenda 20mph (mwendo wa maili 20 kwa saa; wakati sasa magari yamewekewa kwenda 30mph).

2. Kuongeza malipo ya wafanyakazi wa kima cha chini kuwa £7.20.

Jina:

Brian Paddick (mgombea uchaguzi kutoka: Liberal Democrats).

Mapendekezo yake:

1. Kutokomeza silaha za hatari mitaani.

2. Kuongeza huduma za mabasi ya London.

Jina:

Boris Johnson (mgombea uchaguzi kutoka: Conservative Party).

Mapendekezo yake:

1. Kuwapatia polisi wa mitaani vyombo vya kumtambua mtu aliye na silaha mitaani.

2. Kuendeleza mfumo wa 'Congestion Charges' wa London.

Huyu ndiye Meya wa sasa wa London

Jina:

Ken Livingstone (mgombea uchaguzi kutoka: Labour Party).

Mapendekezo yake:

1. Kujenga nyumba 50,000 za rahisi katika miaka mitatu ijayo.

2. Kutokomeza 'Congestion Charges' kwa gari zinazotumia lita ndogo za petroli.

Je, nani unamtaka awe Meya wa London Mei mosi? bonyeza hapa kuangalia sehemu ya karibu na kwako ya kupigia kura.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©