![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Kikwete akutana na Museveni mjini Entebbe, Uganda30/04/2008
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika ikulu ya Entebbe jioni hii. Rais Kikwete na rais Museveni wazungumzia kuhusu Burundi mchana wa leo hii (Aprili 30, 2008) moja kwa moja baada ya kuwasili mjini Entebbe, Uganda, na kuingia katika mazungumzo ya faragha na Rais Yoweri Museveni wa Uganda katika Ikulu ya Entebbe. Rais Kikwete amewasili Uganda akitokea Addis Ababa, Ethiopia ambako alikuwa kwa siku tatu kwa shughuli za nafasi yake kama Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU). Mazungumzo kati ya rais Kikwete na Museveni kwenye ziara hiyo ya kikazi ya siku mbili, yanahusu hali ilivyo katika Ukanda wa Maziwa Makuu, na hasa kwa upande wa Burundi. Rais Museveni ndiye Mwenyekiti wa hali ya Ukanda wa Maziwa Makuu, na Rais Kikwete ndiye Makamu Mwenyekiti. Pamoja na kujadiliana kuhusu hali ya jumla ya Ukanda wa Maziwa Makuu, viongozi hao wawili walisisitiza hasa hali ya amani na usalama katika nchi ya Burundi. Katika siku za karibuni, waasi wa kikundi cha PALIPHEHUTU-FNL wameanzisha tena mashambulizi dhidi ya majeshi ya Burundi, na dhidi ya mji mkuu wa nchi hiyo wa Bujumbura, kinyume cha makubaliano ya amani kati ya pande hizo mbili. Kabla ya kuwasili mjini Entebbe, Rais Kikwete alikuwa Ethiopia ambako alishiriki katika shughuli za AU, ikiwa ni pamoja na kushuhudia makabidhiano ya madaraka kati ya uongozi wa zamani wa Kamisheni ya AU na ule upya. Kamisheni ya Afrika ndiyo huendesha shughuli za siku kwa siku za AU. Katika makabidhiano hayo, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU, Alpha Omar Konare wa Mali alimkabidhi madaraka ya kuendesha Kamisheni hiyo Mwenyekiti mpya, Jean Ping wa Gabon Jumatatu wiki hii katika sherehe iliyofanyika Makao Makuu ya AU mjini Addis Ababa. Mbali na kushuhudia na kusimamia makabidhiano hayo, Rais Kikwete pia alihudhuria kikao cha Kamisheni ya Amani na Usalama ya AU ambacho kilizungumzia migogoro ya Afrika.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||