Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Air Tanzania yapewa mbawa na Serikali

04/01/2009

Serikali imetoa Sh. bilioni 2.5 kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ikiwa ni fedha za awali za kuendesha kampuni hiyo na kulipa baadhi ya madeni kati ya Sh bilioni 3.3 zilizoombwa na kampuni hiyo kama mtaji wa haraka.

Sambamba na hilo, Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa ameunda Tume na kuitaka ifanye kazi kwa siku 21 tangu Desemba 29, mwaka jana ili kubainisha kiini cha matatizo ya ATCL baada ya ripoti ya Bodi ya kampuni hiyo kutotoa maelezo ya kutosheleza.

Mwenyekiti wa Tume hiyo ya watu saba ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi, Profesa Idrissa Mshoro na wajumbe wengine sita, alisema hayo Dk. Kawambwa.

Kuhusu mtaji huo wa Sh bilioni 2.5, Dk. Kawambwa aliwaambia waandishi wa habari jana Dar es Salaam kuwa serikali imeamua kuibeba ATCL kuanzia mtaji mpaka ulipaji wa madeni kwa kuwa ni mmiliki wa kampuni hiyo na kwamba itatoa fedha kwa awamu kulingana na mahitaji ya wakati ya kampuni hiyo.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©