Mashindano ya usanifu wa
basi jipya la LONDON
06/01/2009

Baada ya mamlaka ya London kuamua
kutangaza mashindano ya kusanifu uchoraji wa mabasi mapya ambayo
yatahudumia wakazi na watalii wa London katika jitihada za kubadilisha
mabasi maarufu yaliyopo hivi sasa ambayo yakijulikana kama (London Bus
au Red Bus au Double Decker au Routemaster), vigogo vya usanifu
walioshiriki katika mashindano hayo yaliyoitwa "Imagine a bus for
London", wamejipinda na kujipindua kuleta ufanisi wa sura mpya ya mabasi
hayo ambayo yatabadilisha uso wa mitaa ya London.
Mashindano hayo yalikuwa katika aina nne
za washindani. Washindani wa umri chini ya miaka 11, 11-16, 16-18 na 18
na zaidi.
Maombi 475 ya washindani yalipokewa kutoka
sehemu mbalimbali za UK.
Washiriki waliombwa wabuni mabasi ambayo
yatashabihi miundo ya karne mpya (21st Century) kikamilifu kila pembe
kwa utondoti na kwa yule atakayefaulu kaahidiwa ubunifu wake
utachukuliwa kwenye kiwanda kikubwa kilichotayarishwa cha kutengeneza
mabasi mapya ya London ambapo sura hiyo itabidilishwa kutoka kwenye
picha kuwa basi hai.
Picha nyingi zilizoingia kwenye mashindano
hayo ni picha mbili tu zilizoshinda kwa kuchukuwa nafasi ya kwanza.
Washindi waliosanifu picha hizo wamezawadia £25,000 kila mtu na ubunifu
wa ndio utakaochukuliwa kutengenezwa mabasi mapya ya London.

Mshindi wa Kwanza: Alan Ponsford (57) wa
Capoco Design Limited, UK. £25,000.

Mshindi mwingine wa Kwanza: Aston Martin
and Foster + Partners, London. £25,000.

Mshindi anayefuata: Hector Serrano Studio
na Minarro Garcia wa (UK na Spain). £10,000.

Mshindi anayefuata: Jamie Martin, UK.
£10,000.

Mshindi anayefuata: LA:UK Design Ltd, UK.
£2,000.

Mshindi anayefuata: Concrete All Round
Creative, Belgium. £2,000.

Mshindi anayefuata: Lotti Duke, UK.
£1,000.
-
Mabasi mapya ambayo yatatengenezwa
kufuatia ubunifu wa mshindi wa kwanza Capoco, yataendeshwa kwa
kutumia Hydrogen (kwa nguvu ya umeme) badala ya kutumia Diesel.
-
Yatakuwa na viti vya ziada vya watu
wanne (4) zaidi ya mabasi ya zamani na ukumbi wa watu thelathini
(30) wa kusimama wima.
-
Dereva na Kondakta watawasiliana kwa
kutumia vifaa vya kupaza sauti visivyo na waya (wireless headsets).
-
Gharama ya mabasi mapya yanatarajiwa
kugharimu £150,000.

Routemasters zikionekana zikiwa katika
mtaa wa Oxford Street, London, 1947.
|