Jaji Mkuu aapisha maofisa
wapya
15/01/2009

Jaji mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan
akimwapisha Bw. John Mgeta kuwa Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama Rufani
Tanzania leo katika ukumbi wa mahakama ya rufaa Tanzania jijini Dar es
salaam. Upande wa kulia wa jaji mkuu ni Kaimu jaji kiongozi kanda ya Dar
es salaam Aristoclas Kaijage.

Bw. Huruma Shaidi akipeana mkono na Jaji
Mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhani mara baada ya kuapishwa na kupokea
hati ya uteuzi kuwa Kaimu Naibu Msajili wa Mahakama kuu, Kitengo cha
Biashara Mwanza leo jijini Dar es Salaam.

Jaji mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan
akipeana mkono na Bi. Happines Ndesamburo mara baada ya kuapishwa kuwa
Kaimu Naibu Msajili wa Kitengo cha Biashara Mahakama kuu kanda ya Arusha
katika sherehe fupi iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mahakama ya Rufaa
jijini Dar es salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania Agustino Ramadhan
(mstari wa mbele katikati) katika picha ya pamoja na maofisa wa mahakama
(waliosimama mstari wa nyuma) mara baada ya sherehe fupi ya kuwaapisha
kushika nyadhifa mbalimbali leo jijini Dar es salaam.
|