Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Nafasi za Silisila za programu ya TV

17/01/2009

Kampuni ya Ricochet ambayo inaendesha michezo mbalimbali ya TV nchini UK (ikishirikiana na Channel 4), wametoa fursa ya mtu au gurupu la watu au familia ya kizazi cha pili au kizazi cha tatu au waliohamia UK wakiwa wadogo au waliozaliwa UK lakini wanatamani maisha ya nyumbani kwao wanapotoka (aidha bara la Asia, Marekani, Afrika au Australia au India au Caribbean), wachukue fursa ya silisila ya TV ambayo malengo yake ni kusaidia mtu au watu au familia kufikia malengo yao ya kurudi wanapotoka wazee wao.

Silisila hiyo ambayo itaitwa "Reverse Migration" itamfuatilia mtu atakayechukua fursa hii kuanzia mwanzo anapotoka hapa mpaka anapofika na kusaidiwa kila njia, mfano, kupata kazi anayoikusudia au kuanzisha biashara anayoikusudia ili aweze kuanza maisha yake mazuri, kukodisha nyumba, kama ni familia na watoto, kutafuta shule na kuanza biashara ya maendeleo na familia.

Ufuatao ni mfano uliotungwa na mhariri:

Bwana Boribo kaja UK mwaka 1932, baada ya muda kaoa mke kutoka nyumbani anapotoka (Asia, Afrika, Marekani, Caribbean, n.k.) na kuzaa watoto.

Mwaka 1977 Bwana Maganda (mtoto wa Bwana Boribo) kaoa na kubahatika kupata watoto wawili, Korosho na Unga.

Mwaka 2008 Bwana Korosho (mjukuu wa Bwana Boribo) anatamani kuishi maisha yenye mila, utamaduni na asili ya anapotoka babu yake bwana Boribo, lakini Bwana Korosho hajui aanze wapi kimaisha na biashara ya kumuendeshea maisha yake atakapofika nyumbani anapotoka babu yake. Ricochet inamsaidia yeye na familia yake yote katika silisila hii kwenda nae hatua kwa hatua na kumsaidia mpaka apate nyumba ya kuishi na watoto wake, kazi au msingi wa biashara, shule ya watoto wake na mpaka kujisikia kuwa yupo nyumbani. Mwishowe, Bwana Maganda anapata msingi mzuri wa kuanza biashara yake, shule ya watoto wake kusoma na anaishi maisha aliyokuwa akiyatamani kuishi miaka yote. Tamati.

Mfano wa pili:

Kibwenzi kaja UK mwaka 1995 akiwa na miaka 10.

Mwaka 2008 anatamani kurudi nyumbani kuishi maisha yenye mila, utamaduni na asili ya nyumbani anapotoka, lakini hana uwezo wa kurudia nyumbani na hajui akirudi aanze wapi kimaisha na biashara au kazi ya kumuendeshea maisha yake atakapofika nyumbani alipotoka. Ricochet inamsaidia katika silisila ya TV kwenda nae hatua kwa hatua na kumsaidia mpaka apate nyumba ya kuishi na kazi au biashara ya kujiendeleza na maisha yake na mpaka kujisikia kuwa yupo nyumbani. Mwishowe, Kibwenzi anapata msingi mzuri wa kuanza biashara na anaishi maisha aliyokuwa akiyatamani kuishi miaka yote. Tamati.

Utafiti uliofanyika IT City, mjini Bangalore, India, umeonyesha kuwa wafanyakazi si chini ya elfu arobaini (40,000) ambao wanafanya kazi IT City, India, wametoka aidha UK au US wameamua kurudi nchini kwa kikazi na kuanza maisha mapya.

Mwisho wa safari hii na Ricochet, uamuzi ni wa familia au mtu atakayechukua fursa hii kubaki nyumbani kwenye asili yao au kurudi UK na kuendelea maisha ya UK.

Kwa atakayependelea kuchukuwa fursa hii, piga simu 01273 224816 wasiliana na Sophie Chandler (Muendeshaji Msaidizi, Ricochet) au email: sophie.chandler@ricochet.co.uk

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©