Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

US Airways yaanguka mtoni (Hudson River)

18/01/2009

Chelsey Sullenberg, pichani, ni rubani wa shirika la ndege la US Airways ambaye alithibitisha kuwa ni kapteni na shujaa wa ndege aina ya Airbus 320 namba 1549 iliyoruka kutoka uwanja wa ndege wa LaGuardia uliopo New York kuelekea mji wa Charlotte, North Carolina siku ya Ijumaa ya tarehe 16/01/2009.

Ushujaa wake ulikuja baada ya kuishusha ndege hiyo kwenye mto wa Hudson uliopo Manhattan, New York, mara baada ya kupatwa na ajali na kuokoa maisha ya watu wote 155 waliomo ndani ya ndege hiyo.

Bwana Chelsey ana uzoefu wa kurusha ndege za abiria usiopungua miaka 29 na kabla ya hapo alikuwa rubani wa ndege za kivita za US Airforce.

Mara baada ya kuruka uwanja wa ndege wa LaGuardia, bwana Sullenberg alihisi tofauti ya mwenendo wa ndege yake na mwisho kutambua kuwa injini zote mbili za ndege zilikuwa zipo katika hali ya utata na isitoshe moja ilikuwa ishaanza kuwaka moto.

Uwanja wa ndege wa karibu wa kuitulisha ndege hiyo ulikuwa mbali naye na hakuwa na khiyari bali kuishusha ndege hiyo kwenye maji ya mto wa Hudson (Hudson River), magharibi mwa mji wa Manhattan.

Mara baada ya kutua salama na kuokoa watu wote waliokuwamo kwenye ndege hiyo, bwana Sullenberg alitembea kutoka jikoni alipo mpaka kwenye mkia wa ndege kuhakikisha watu wote wametoka kwa usalama na hakujabaki mtu ndani ya ndege hiyo.

Inasemekana ajali hiyo ilisababishwa na ndege wakubwa aina ya bata warukao angani kuingia kwenye injini ya ndege mnamo saa 3.26pm sekunde 30 au 45 baada ya kuruka tu kutoka uwanjani. Shujaa huyo kapongezwa na viongozi mbalimbali wa nchini Marekani katika sakata hilo lililoitwa "Miracle on the Hudson".

Mawasiliano baina ya Rubani na muongoza njia za hewa bonyeza hapa chini.

Angalia filamu iliyotengenezwa hai ya tukio hilo kwa kubonyeza hapa chini.

Angalia filamu ya kweli iliyokamatwa na CCTV ya Coast Guard kwa kubonyeza hapa chini.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©